25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Makamu wa Rais,mkewe waambukizwa corona

 JUBA, Sudani Kusini

MAKAMU wa Rais wa kwanza wa Sudani Kusini, Riek Machar na mke wake, Angelina Teny wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Dk. Machar alisema yeye na mke wake ambaye pia ni waziri wa ulinzi, wamepata maambukizi, baada ya kutangamana na jopo la ngazi ya juu la kukabiliana na virusi hivyo nchini humo.

Machar alisema hana dalili zozote na hali yake ya afya iko sawa,lakini atajiweka karantini kwa siku 14.

Wengine waliothibitishwa kuambukizwa ni walinzi kadhaa na wafanyakazi. Mpaka sasa Sudan Kusini, imerekodi waathirika 236 na vifo vinne.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake: “Bado tunasubiri matokeo mengi na ni matumaini yetu kwamba kesho, tutakuwa na orodha kamili ya walioambukizwa katika jopo hili,” Machar amezungumza hayo katika mkutano na wanahabari uliofanyika Jumatatu mjini Juba…Huenda daktari akatutembelea hadi atakapotuarifu kwamba wakati umewadia wa kumaliza karantini’’.

Wiki wiki iliyopia, maofisa walitangaza virusi hivyo vimefikia kwenye kambi ya waliotoroka makazi yao ambao wamekuwa wakiitaka Umoja wa Mataifa iwalinde katika mji mkuu wa Juba tangu 2013.

Nchi hiyo bado inakabiliana na baa la njaa hata baada ya Machar na Rais Salva Kiir — waliokuwa mahasimu kuunda serikali ya umoja wa taifa Februari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles