24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Makamu wa Rais, mgeni rasmi uzinduzi kampeni ya kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kuzuia Vifo Vitokanavyo na Uzazi na Watoto Wachanga.

Kampeni hiyo iliyopewa kauli mbiu  ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ itazinduliwa Novemba 6, mwaka mkoani Dodoma.

Hayo yameelezwa leo Novemba Pili na Daktari Mwandamizi, Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Phineas Sospeter alipokuwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari kuhusu kampeni hiyo.

Amesema kampeni hiyo imelenga kukabili, kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ambavyo takwimu zinaonesha vipo juu.

“Takwimu zilizopo zinaonesha kuna vifo vya uzazi 556 katika kila vizazi hai 100,000 na vifo vya watoto 25 kwa kila vizazi hai 1,000,” amesema.

Dk. Sospeter amesema lengo la Serikali ni kupunguza vifo hivyo kufikia 292 kwa kila vizazi hai 100,000 na vifo 16 kwa kila vizazi 1,000 kwa upande wa watoto.

“Kampeni hii haijaacha kundi hata moja, tutahusisha viongozi wa serikali, dini na wananchi moja kwa moja, ili kuweza kufikia lengo hill,” amesema

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles