32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Makamu wa Rais Cuba kuzuru nchini

MAKAMU wa Rais wa Baraza la Taifa la Jamhuri wa Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa
MAKAMU wa Rais wa Baraza la Taifa la Jamhuri wa Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa

Na JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM

MAKAMU wa Rais wa Baraza la Taifa la Jamhuri wa Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa, anatarajia kufanya ziara ya siku tatu nchini kuanzia Oktoba 2 hadi 4, mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Augustine Mahiga, katika mkutano wake na waandishi wa habari jana Dar es Salaam.

Dk. Mahiga alisema ziara hiyo itakayoanzia Tanzania bara na baadaye kuelekea Zanzibar, ina lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na nchi hiyo pamoja na kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta ya uwekezaji.

Alisema moja ya ajenda kuu katika mkutano wa viongozi na Mesa ni kuangalia namna Cuba itakavyosaidia kuendeleza na kuangalia jinsi ya kuwa na kilimo cha kisasa cha zao la miwa.

“Suala la uwekezaji katika kilimo hususani cha miwa litakuwa kwenye mazungumzo hasa ukizingatia Cuba ni moja ya nchi duniani zinazoongoza kulima miwa hivyo tutakuwa hatujatumia ziara hii vizuri kama tutaacha kujadili suala hili.

“Pia ni moja kati ya nchi ambazo zimekuwa zikitoa mchango mkubwa kwa nchi hususani kwenye sekta ya afya na hadi sasa imetupatia madaktari 30 ambao wapo katika hospitali mbalimbali bara na visiwani.

Alisema kati ya madaktari hao 30, madaktari 10 wapo bara na 20 Zanzibar wakiwemo wakufunzi katika Kitivo cha Tiba na Chuo Kikuu cha Zanzibar.

Alisema katika upande wa sekta ya elimu, Cuba imekuwa ikifadhili wanafunzi wa hapa nchini kwenda kusoma ambapo kuanzia 2008 hadi 2014 ilifadhili Watanzania 64 katika mafunzo ya udaktari, uchumi, Tehama na michezo.

“Pia Tanzania na Cuba ilianzisha programu ya elimu kwa vijana na watu wazima ambayo hutolewa kwa kutumia vifaa vya kufundishia vinavyomwezesha mwanafunzi kusikia na kuona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles