27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Makamu wa Rais atangaza kuwa na virusi vya corona

JUBA, SUDAN KUSINI

MAKAMU wa Rais wa Sudan Kusini Dk. James Wani Iga amesema amebaini kuwa ana corona baada ya kufanyiwa vipimo.

Akitangaza taarifa hiyo kupitia Shirika la Habari la Taifa la Sudan Kusini alisema: “Sampuli zangu zilichukuliwa siku chache zilizopatikana na leo nimepatikana na ccorona…kwa hiyo ninawaomba raia wote wa Sudan Kusini kwenda kupimwa, hii ni muhimu ili tupunguze kusambaa kwa virusi kwa watu wengi,” alisema .

Taarifa ya kupatwa kwa maambukizi ya virusi vya corona kwa Dk. inakuja baada ya viongozi wengine wakuu wa nchi hiyo kutangaza kupatwa na Covid-19 akiwemo makamu rais wa nchi hiyo, Riek Machar na mkewe ambao pia waliambukizwa virusi vya corona mwezi huu.

Miongoni mwao ni Dk. Machar aliyesema kwamba yeye na mke wake ambaye pia ni waziri wa ulinzi, walipata maambukizi baada ya kutangamana na jopo la ngazi ya juu la kukabiliana na virusi hivyo nchini humo.

Wakati huo Machar alisema kwamba hana dalili zozote na hali yake ya afya iko sawa lakini atajiweka karantini kwa siku 14.

Walitangaza kwamba virusi hivyo vimefikia kwenye kambi ya waliotoroka makazi yao ambao wamekuwa wakiitaka Umoja wa Mataifa iwalinde katika mji mkuu wa Juba tangu 2013.

Nchi hiyo bado inakabiliana na baa la njaa hata baada ya Machar na Rais Salva Kiir,  waliokuwa mahasimu kuunda serikali ya Umoja wa Taifa Februari.

Viongozi hao wawili bado hawajakubaliana masuala ya msingi kama udhibiti wa majimbo.

Wengine waliothibitishwa kuambukizwa ni walinzi kadhaa na wafanyakazi.

Mawaziri 10 tayari wameambukizwa virusi vya corona nchini humo, kulingana na taarifa iliyotolewa mwezi huu na msemaji wa serikali katika mahojiano na BBC.

Waziri wa Habari wa Sudani Kusini, Michael Makuei aliiambia BBC kuwa mawaziri wote hao walikuwa ni wajumbe wa kamati ya juu ya serikali ya kupambana na corona nchini humo.

Katika mawaziri waliopo kwenye kamati hiyo, ni Waziri wa Afya pekee ambaye hakukutwa na maambukizi.

Iliripotiwa kuwa mawaziri hao waliambukizwa Covid-19 baada ya kukutana na aliyekuwa mjumbe wa kamati hiyo ambaye alikuwa na virusi vya corona.

Mawaziri wote 10 walijitenga kwa sasa na serikali imesema kuwa wote wanaendelea vizuri kiafya.

Walinzi wa viongozi kadhaa nchini humo pia walikutwa na virusi na na kuwekwa karantini.

Mpaka sasa zaidi ya watu 300 wamethibitishwa kupata corona Sudani Kusini, huku watu wane wakipona na sita kufariki.

Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya hatari ya kuporomoka kabisa kwa mfumo wa afya wa nchi hiyo ambao una uwezo mdogo kutokana na mgororo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambao umeathiri ustawi wa maendeleo.

Kwa sasa Rais Kiir ameweka tofauti zao za kisiasa kando na kutengeneza serikali ya umoja wa kitaifa, japo hawajaweza kukubaliana katika baadhi ya mambo ya msingi kama udhibiti wa majimbo.

Wakati corona ikiendelea kuleta wasiwasi, nchi hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa chakula kwa sasa.

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles