31.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 31, 2023

Contact us: [email protected]

MAKAMBO, FEI TOTO KUANZA KAZI YANGA LEO

NA WINFRIDA MTOI


STRAIKA mpya wa Yanga, Heritier Makambo na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’, wanatarajia kuonekana uwanjani leo wakati miamba hiyo ya Jangwani itakapoumana na Mawenzi FC, katika mchezo wa kujipima nguvu utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Yanga, mbali ya kupima makali yake, pia itautumia mchezo huo kumuaga nahodha wa muda mrefu wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ambaye ameamua kustaafu soka.

Makambo alisajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati Feisal akitokea JKU ya Zanzibar.

Nyota hao wawili walianza mazoezi na timu yao hiyo mpya siku kadhaa zilizopita, lakini hawakuwahi kuichezea mechi yoyote dhidi ya timu pinzani.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten, alisema mbali ya wakali hao, kipa wao mpya, Klaus Kindoki naye atasimama langoni kwa mara ya kwanza.

Alisema kabla ya kushuhudiwa kipute cha Yanga na Mawenzi, litatanguliwa pambano kati ya timu ya wanawake ya Yanga Princes itakayoumana na  Morogoro Women, huku ikitarajiwa pia kutolewa burudani ya muziki.

“Tumeandaa bonanza hili maalumu litakaloanza saa 3:00 asubuhi, kwa lengo la kumuaga na kumshukuru Cannavaro, kwa sababu ni mchezaji aliyefanya vitu vingi na Yanga, tunataka atambue kuwa Wanayanga wanathamini mchango wake,” alisema Ten.

Aliwataja wasanii watakaotumbuiza leo kuwa ni   Juma Kassim ‘Nature’, Msaga Sumu, Mr Blue, Gigy Money, Afande Sele, Dollo, Rich One, Lulu Diva na Bill Nas.

Wakati huo huo, Ten alisema wachezaji Ibrahim Ajib, Papy Tshishimbi na Ramadhan  Kabwili wataungana nao leo Morogoro.

Alisema wachezaji hao watatu walishindwa kuambatana na timu juzi kutokana na matatizo tofauti ya kifamilia.

Alisema pia klabu hiyo imemalizana na aliyekuwa kipa wa timu hiyo, Youthe Rostand, ambaye hivi karibuni waliafikiana naye kuvunja mkataba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles