25.3 C
Dar es Salaam
Monday, January 17, 2022

MAKALLA AWAPA SOMO VIONGOZI WA VIJIJI, KATA

Na PENDO FUNDISHA-MBEYA


WATENDAJI wa vijiji, kata na wataalamu wa halmashauri, wametakiwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za uhamishaji wa makao makuu ya ofisi za Serikali, ili kupunguza migogoro isiyokuwa ya lazima kwa wananchi.

Hayo yameelezwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla, wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Ilembo Inyara, Shisieta na Insonso, vilivyopo wilayani Mbeya.

Katika mazungumzo yake, Makalla alisema alilazimika kuyasema hayo baada ya kuibuka kwa mgogoro kati ya wananchi wa Kijiji cha Ilembo Inyara na Shisieta, wanaogombania eneo la kujenga ofisi za kata.

Alisema kwamba, ofisi za Serikali hazihamishwi kiholela bali ni lazima zifuate utaratibu hasa zile zinazohamisha makao makuu ya mji kutoka kijiji fulani kwenda kijiji kingine.

“Suala hili limetajwa hata katika Katiba ya nchi na wote lazima tuheshimu Katiba yetu kwani si ya CCM wala Chadema bali ni Katiba ya Tanzania.

“Katiba ya nchi yetu imeeleza madhumuni ya kuweko kwa Serikali za Mitaa na lengo lake ni kupeleka madaraka kwa wananchi na kutoa haki ya kupanga mipango na shughuli za maendeleo.

“Lakini ukiangalia mchakato uliofanyika wa kuhamisha ofisi ya mtendaji kata kutoka Kijiji cha Ilembo Inyara kwenda Shisieta, unaona umeghubikwa na changamoto nyingi zinazohitaji kutatuliwa.

“Pamoja na hayo, nawaomba wananchi wa vijiji hvi, kamati za maendeleo za kata na baraza la madiwani, kutoa mapendekezo yenu pamoja na wataalamu wa halmashauri waangalie jiografia ya mahala pa kuweka ofisi hizo na si kukurupuka,” alisema Makalla.

Pamoja na hayo, aliwahakikishia wananchi wa vijiji hivyo kwamba Serikali ya Mkoa wa Mbeya na wilaya, zitaratibu zoezi hilo la uhamishaji wa ofisi ya kata ili haki itendeke na watu wa pande zote waridhike.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,717FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles