Na Brighter Masaki, Mtanzania Digital
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewaomba madiwani na Wenyeviti wa mtaa kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha jamii katika suala la usafi.
Makalla ameyasema hayo leo Jumanne Juni 15, 2021 katika kikao cha madiwani na watendaji kata manispaa ya Temeke katika ziara yake ya kujitambulisha na kueleza vipaumbele kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Amewaeleza madiwani na watendaji nanma ambavyo haridhishwi na hali ya usafi Dar es Salaam na kuwaomba kumuunga mkono kuiliweka jijii Safi.
Aidha, Makalla ameeleza mpango wake wa kupendezesha mandhari ya mkoa, kuwapanga vizuri wamachinga na kuondosha magari mabovu yanayoharibu mandhari ya Jiji hilo.
Katika kikao hicho Makalla pia amewapa vipaumbele vya kushughulikia ikiwemo ulinzi na usalama, usimamizi miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa Mapato, utatuzi wa kero za wananchi na kuimarisha umoja na mshikamano.