23.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Makalla aendesha harambee ya kumchangia Lissu atengeneze gari lake

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla, ameendesha harambee ya kuchangia gharama za kutengeneza gari la Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu. Harambee hiyo imefanyika leo Alhamisi, Agosti 15, 2024, katika Uwanja wa Furahisha, jijini Mwanza, wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM, ambapo jumla ya Shilingi milioni 5.3 zimepatikana.

Tundu Lissu.

Makalla aliamua kuendesha harambee hiyo wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi, akieleza kuwa aliguswa na hali ngumu anayopitia Lissu, hasa kutokana na taarifa zilizotolewa na kada wa zamani wa Chadema, Mchungaji Peter Msigwa. Msigwa alieleza kuwa wakati viongozi wengine wa Chadema wakisafiri na msafara mkubwa wa magari, Lissu amekuwa akitumia gari moja bovu pamoja na walinzi wake licha ya hali aliyonayo.

“Nimesikitishwa sana na Lissu kuendeshwa kwenye gari bovu. Nimesikitishwa sana, naomba tumchangie, mwenye kuchangia chochote alete hapa,” alisema Makalla, akiongeza kuwa Lissu ni ndugu yake kutoka Singida na kwamba alikuwa na nia ya kumsaidia.

Katika harambee hiyo iliyochukua dakika 15, kiasi cha Shilingi milioni 5.3 kilipatikana, ambapo fedha hizo zitawekwa moja kwa moja kwenye akaunti ya Lissu na risiti ya muamala huo itakabidhiwa kwake kama ushahidi wa mchango huo kutoka kwa wanaCCM.

Akizungumza baada ya kufahamishwa kuhusu harambee hiyo, Lissu aliwashukuru CCM kwa mchango huo na alieleza kuwa atazipokea fedha hizo kama ambavyo amekuwa akipokea michango kutoka kwa makundi mbalimbali ya watu.

“Nawashukuru, kama nilivyosema… hatukusema tunachangiwa na wanaChadema peke yao. Kama nilivyotibiwa, sikutibiwa na wanaChadema peke yao. Kwa hiyo, wakichangia nitazipokea, sina sababu ya kukataa,” alisema Lissu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles