25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

Makali ya Skillager kwenye ‘busy body’ usipime

Na Joseph Shaluwa

MWANAMUZIKI anayekuja kwa kasi kwenye game ya Afro Pop, Felix Philemon Sola ‘Skillager’ ameachia kitu kipya, ‘Body Busy’.

Msanii huyo ambaye licha ya kuimba ni mtumbuizaji na mwandishi wa mashairi, ameachia jiwe hilo moto, akiwa chini ya Lebo ya Tree of Life Entertainment ya nchini Nigeria.

Wimbo huu wa kusisimua ni heshima kwa wanawake wa Kiafrika, ukiakisi kusherehekea nguvu, urembo na ujasiri wa mwanamke wa Kiafrika.

‘Busy Body’ unazungumzia shamrashamra za wanawake wa Kiafrika, ambao mara nyingi ndio nguzo ya familia na jamii zao.

Utundu wa kipekee wa Skillager na mtazamo mpya unamfanya kuwa kinara katika ulimwengu wa muziki wa Afro Beat.

Muziki wake unazungumzia juu ya mapambano na ushindi wa watu wa kila siku, huku ukisisitiza watu kutokuwa wabaguzi.

Tayari kibao hicho, ‘Busy Body’ kinapatikana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii inayodili na muziki, hivyo basi tembelea sasa ili kutoa sapoti kwa staa huyu ajaye, lakini pia kupata ladha ya aina yake kwa mwanamuziki huyu anayekuja kwa kasi ya kimbunga.

Msanii huyu ni mzaliwa wa Jimbo la Adamawa, akiwa amekulia Ebonyi, kusini kwa Nigeria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles