24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Makala: Zaina Neema kutoka Canada Christina Shusho, Rose Muhando, Joel Lwaga

Montreal, Canada

MIAKA ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la Waimbaji wengi wanaofanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili, miongoni mwao, Zaina Neema ambaye ni muimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Canada.

Karibu www.mtanzania.co.tz ufuatilie mazungumzo haya ili umfahamu vizuri, Zaina Neema ambaye kwa sasa anatamba na wimbo, Wewe na Mimi unaochezwa kwenye runinga mbalimbali.

SWALI: Kwa kifupi Zaina ni nani na uliingia vipi kwenye sanaa ya muziki?

Zaina: Mimi ni msanii wa Gospo kutoka Canada kwenye Mji wa Montreal pia naimba, mtunzi wa dansi mwenye asili ya Tanzania na Congo RDC na kupitia muziki nimekuwa nikipenda kusambaza ujumbe wa upendo na amani ya moyo.

SWALI: Kuna changamoto zozote unazopata kufanya sanaa ya muziki nchini Canada?

Zaina: Kufanya muziki nchini Canada haswa kwa sisi ambao hufanya muziki wa injili sio rahisi kabisa lakini asante Mungu tunajaribu kufika huko bila shaka tutakua zaidi kwenye eneo hili la Canada na huko Afrika.

SWALI: Wasanii gani unatamani kufanya nao kazi kutoka hapa Afrika Mashariki hasa Tanzania?

Zaina: Wasanii ambao ningependa kushirikiana nao na nina thamini sana kazi zao ni Joël Lwaga, Christina Shusho na GoodLuck Gozbert na Rose Muhando.

SWALI: Mpaka sasa umepata mafanikio gani kwenye sanaa?

Zaina: Nimekuwa nikiimba muda mrefu lakini mwaka huu nilipata maoni ya kitaalam ya kuweza kufanya kazi na wasanii wengi. Nashukuru Mungu nilifanya kazi na Joël Mbenza wimbo unaitwa Ushindi ambao ulipendwa sana na ukanifungulia milango zaidi.

SWALI: Ujumbe gani ulitaka uwafikie mashabiki kupitia wimbo wako Wewe na Mimi?

Zaina: Ujumbe ambao ningependa kuwapa watu kupitia nyimbo yangu ni kwamba Mungu ni upendo, ndani ya Wewe na Mimi kuna ujumbe wa upendo wangu Mimi na Mungu ambao unafanya tunatimiza mambo mazuri kwa wengine hapa duniani.

Pia nyimbo zangu zinapatikana kwenye majukwaa yote ya kupakua na kusikiliza muziki kama vile YouTube, Spotify, iTunes, Apple Music na Deezer au kwa kufuata link hii https://ampl.ink/nREpY.

SWALI: Tumeingia nusu ya pili ya mwaka 2021, je umewaandalia nini mashabiki wako?

Zaina: Tuna projekti nyingi sana mimi na timu yangu, nina uhakika kwamba mwaka huu kabla ya kumalizika zitasikika hapa Canada na huko Afrika.

Siwezi kuahidi lini zitatoka lakini kaa chonjo katika wiki zijazo utakuwa unasikiliza wimbo wangu mpya ila kwa sasa unaweza kuingia YouTube na kutazama video ya Mimi na Wewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles