27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Makala: Geita mji wanavyopambana kupanua wigo uzazi wa mpango

Na Yohana Paul, Geita

MATUMIZI ya uzazi wa Mpango ni miongoni mwa huduma ya afya ya uzazi ambayo kwa siku za hivi karibuni imekuwa ikisisitizwa sana ulimwenguni kote hususani katika nchi za bara la Afrika, Tanzania ikiwa mmoja wapo kulenga kukabiliana na athari zitokanazo na ongezeko la watu.

Baadhi ya athari hizo ni pamoja na ukataji miti kwa kiwango kikubwa kwa ajili ya ujenzi wa makazi hali inayopelekea maeneo mengi yenye uoto na misitu ya asili kuwa katika hatari ya kugeuka majangwa, ongezeko la magonjwa ya mlipuko, misongamano katika vituo vya kutolea huduma za kijamii ikiwemo shule na vituo vya afya.

Ili kuenenda na adhima ya kuongeza  matumizi ya uzazi wa mpango, halmashauri ya mji wa geita mkoani Geita kwa kipindi cha miaka mitatu sasa ipo kwenye utekelezaji wa mradi wa utoaji elimu ya uzazi wa mpango, kupunguza mimba za utotoni na huduma ya uzazi kwa vijana.

Akielezea mwenendo wa matumizi ya uzazi wa mpango mjini Geita, Muuguzi Mkuu Halmashauri ya mji wa Geita, Caritus Ntambi anasema hadi sasa kiwango cha matumizi ya uzazi wa mpango katika halmashauri ya mji wa Geita imefikia asilimia 35.3 kiwango ambacho bado ni kidogo ikilinganishwa na uhalisia wa idadi ya watu.

Anasema takwimu zinasema asilimia 25 ya kina mama wanaojifungua wanatakiwa kutumia huduma ya uzazi wa mpango, lakini mpaka kwa walio wengi hawafanyi hivo, na kwa kuliona hilo shirika limeona liongeze nguvu ili watumiaji waweze kuongezeka kwani watumiaji wakiwa wengi hususani kina mama, inawezekana kupunguza vifo vya wajawazito wanaojifungua kwa asilimia 40.

Anasema ili kupanua uwigo wa matumizi ya uzazi wa mpango, mpaka sasa halmashauri hiyo inaendelea na mradi unaofadhiriwa na Shirika la TUPANGE PAMOJA kwa kushirikiana na JAPAIGO ukiwa na malengo makuu matatu, kwanza ni uzazi wa mpango, utoaji huduma rafiki kwa vijan  na lango la tatau ni kupinga mimba za utotoni.

Anasema mikakati hiyo imeanza kufanyika hata kabla ya mradi lakini ujio wa wadau umeongeza mbinu mbadala za kuweza kuwafikia watu wengi zaidi, kama vile wahudumu wa afya kuwafuata ananchi ndani ya jamii, kutenga siku mbili kwa juma kwa ajili ya kutoa huduma za uzazi wa mpango.

“Tunafanya kazi katika vituo 15 ndani ya halmashauri ya mi wa Geita, abavyo vinatoa uduma ya uzazi, na vituo hivi vinahudumia uzazi wa mpango katika jamiii, tunaelimisha jamii juu ya kupinga mimba za utotoni, lakini pia tunatoa elimu juu ya huduma rafiki kwa vijana,” anaeleza.

Ntambi anakiri kuwa changamoto kubwa iliyopo ni ushiriki wa wanaume kuwa bado ni mdogo kwani jami bado inaamini mipango ya uzazi wa mpango ni jukumu la mama pekee ingawa maana halisi ya uzazi wa mpango ni ushiriki wa bab na mama kama familia kukaa pamoja kujadiliana ni lini waanze kuzaa, wazae watoto wangapi ambao watapishana kwa muda gani.

“Kwa maeneo mengi kwa sababu unakuta mama ndio mtumiaji, wakati mwingine wababa wanakataa, unakuta mama katumia kwa siri kwa kujificha, na muda mwinine kushindwa kutumia kwa kuogopa kwamba akitumia mme wake anaweza asimuelewe na akamufanyia kitendo ambacho ni kibaya,”

Anaongeza, malengo ya mradi hadi kukamilika ndani ya kipindi cha miaka mitatu, angalau kupiga hatua kwa asilimia 20 (kufikia asilimia 75) zaidi kutoka kwenye kiwango cha sasa ambacho ni asilimi 35.3 na baada ya hapo halmashauri itaendelea na misingi iliyojiwekea kuendeleza kupanua uwigo zaidi na zaidi.

Akitoa tahimini ya mwamko wa matumizi ya uzazi wa mpango mjini Geita, Afisa Muuguzi halmashauri ya mji wa Geita, Rehema Kitowa anaweka wazi kwamba mradi umeonekana kuzaa matunda kwani kwa tathimini ya haraka inaonyesha idadi ya watumiaji wa huduma ya uzazi wa mpango mji wa Geita inazidi kuongezeka kila mwaka.

“Ukichukua takwimu za mwaka jana na mwaka juzi, tunaamini kwamba katika kipindi cha mwaka 2019 tunaona kwamba matumizi ya uzazi a mpango yalikuwa ni asilimia 29, lakinikwa kpindi cha 2020 tumeweza kupanda mpaka kufikia asilimia 35.3 hii inaonyesha jinsi gani kunaendelea kuwepo na mwamko katika jamii,” anafafanua Rehema.

Anasema mafanikio hayo yamewezesha kupunguza idadi ya vifo vya kina mama wajawazito ambapo juhudi zaidi zinaendelea kufanyika kuhamasisha jamii kupitia wadau mbalimbali kwa kusaidiana na halmashauri ya mji kwani kwa kipindi cha mwaka juzi (2019) vifo vitokanavyo na uzazi vilikuwa 31 na kwa mwaka jana (2020) vifo vya  vya aina hiyo vilikuwa 29 pekee.

“Tunaendelea kutoa huduma ya afya kupitia mashule, lakini vile vile tunaifikia jamii kwa huduma mkoba ambazo zinakuwa zinaendelea katika vituo vyetu, si vituo tu inawezekana kuna eneo linakuwa lipo mbali na kituo basi tunashirikiana na uongozi wa kijiji au kata kuweza kupata sehemu maalumu tunapoweza tukatoa huduma ya uzazi wa mpango,”

Kitowo anasisitiza mbinu mbadala ya ushirikishwaji wa wanaume imewezesha kufikia mafanikio zaidi, na pia utumiaji wa viongozi wa dini na watu maarufu kusimama kama wahamasishaji wa matumizi ya huduma ya uzazi wa mpango sambamba na uanzishwa wa klabu za wa vijana na hadi sasa kuna jumla ya klabu 15 kwa pamoja zimewezesha kutia chachu zaidi.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Elimu na Uchumi, Merry Kasamwa anaunga mkono juhudi zinazofanywa na halmashauri ya mji kupanua uwigo wa matumizi ya uzi wa mpango kwani kwa kushirikisha makundi ya wadau tofauti imeonyesha kuleta matokeo chanya katika halmashauri ya mji wa Geita.

Mbali na mafanikio yaliyoanza kuonekana anaushauri waratibu wa mradi huo unaofadhiriwa na shirika la TUPANGE PAMOJA kuhakikisha wanaifikisha elimu hiyo maeno ya vijijini kwa kushirikiana na viongozi wa mitaaa na vijiji ambao kwa nafasi yao watasaidia kuelimisha kwani ni ukweli ulio wazi kwamba watu wengi kwenye maeneo hayo hawafahamu chochote juu ya kupanga uzazi.

“Utakuta asilimia kubwa hasa kina mama vijijini wanapata shida sana kwa kuwa na watoto wengi, wababa wanawakimbia wakina mama wanapoona kwamba familia imekua kubwa, lakini wakiwa wamekaa kwa pamoja kupata elimu ya uzazi baba hawezi kuikimbia familia yake , kweli elimu hii inavytolewa hivi sisi tunaona ni tija kubwa  kwa wananchi wetu

“Nafikiri wakipewa elimu hususani jinsi ya kutumia uzazi a mpango wa asili, ile inaweza ikawasadia sana kwa sbabu watu wankuwa na ile dhana potofu ya kusema kwamba wanpotumia vidonge vya uzazi wa mpango (majira) wanazaa wale watoto matahira , walemavu lakini wakipewa ile njia ya asili inaweza ikasaidia sana hususani vijijini,” anasema Merry.

Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Mji wa Geita, Cathbert Byabato anasema makundi makubwa yanayopatiwa elimu ya uzazi wa mpango ni pamoja na masdiwani, watu mashuhuri kutoka mitaa ambao  wataweza kusimama kama waelimishaji ndani ya jamii kam sehemu ya kuongeza uwigo wa uelewa ndani ya jamii.

Anasema kwa halmashauri yake mradi umeweza kutekelezwa kwenye kata saba aambapo ili kusaidia vijana kuwa wawazi na kuongeza ushiriki wao katika masuala ya afya ya uzazi, tayari vituo vyite vya afya vimeagizwa kutenga vitengo maalumu vya kutolea huduma kwa vijana kwa faragha zaidi.

Mbali na elimu ya afya ya uzazi inaotolewa, Byabato anawashauri vijana ambao bado wapo kwenye hatua za masomo kwa maana ya shuleni na vyuoni kuchukua tahadhari kwa kutojiuhusisha na ngono zidixzo salama kwa kufanya hivyo watakuwa siyo tu wamedhibiti mimba a utotoni bali pia watakuwa wamepanga uzazi.

Byabato anahitimisha kwa kuishauri jamii nzima ikiwemo vijana na watu walio kwenye ndoa kuzingatia elimu ya uzazi inayotolewa ili iweze kuwasaidia kupanga uzazi na kupunguza kuzaa pasipo kutarajia kama njia mojawapo ya kufikkia malengo  na maendeleo ya kiuchumi kwenye halmashauri ya mji wa Geita.

“Tunaamini kwamba jamii yetu inahitaji maendeleo, na maendeleo kweli yanatkana na mambo makuu ambayo yanatakiwa yazingatiwe kwamba lazima tuwe katika hari ya ambayo ni bora zaidi ili kuweeza kuwa na mahusiano, tusijiingize atika mahusiano pasipo kuwa tumewekeza kitu ambacho kinaweza kumsaidia yule mtoto,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles