23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MAKAHABA NIGERIA  WATISHIA KUGOMA

 

LAGOS, Nigeria


CHAMA Cha Wanawake wanaofanya biashara ya kujiuza nchini  Nigeria, kimetishia kuitisha mgomo kwa kile ambacho kinadai kuwa wanachama wake wamekuwa wakilazimishwa kufanya ngono na polisi  baada ya kuwakamata na kuwatishia kuwafungulia mashtaka.

Chama  hicho kilisema juzi kuwa asilimia 50 ya wanachama wake wamekuwa wakifanyiwa  vitendo hivyo na polisi katika mji wa Anambra  katika Jimbo la Orumba Kusini.

Mmoja wa wanawake ambaye alijitaja kwa jina moja la  Kaamsi, ambaye pia ni mmoja wa viongozi wa chama cha  Orumba South LGA,  alisema  polisi wamekuwa wakiwafuata katika maeneo yao na kuwabughudhi kabla ya kuwalazimisha kulala nao.

“Polisi hawa wameshawalazimisha asilimia 50 ya wanachama wetu, wamekuwa wakija katika maeneo yetu na kutumbua kila siku.” alisema kiongozi huyo.

“Karibu siku mbili zilizopita  hapa  hakuna wanachama  chini ya 10  kwa sababu  walikamatwa na kupelekwa kwenye ofisi  za polisi. Walikuwa wakitendewa vibaya…. kabla ya kuruhusiwa walilazimishwa kulipa dhamana kwa kutumia miili yao,”aliongeza kiongozi huyo.

Alisema   matukio hayo yamekuwa yakitokea kila siku katika maeneo ya  Umunze, Onitsha, Awka, Nnewi, Ekwulobia na kwamba wamekubaliana hakuna mwanachama yeyote atakayempa huduma polisi katika eneo hilo la  Umunze na mengine katika jimbo hilo.

Alipohojiwa kama askari hao wamekuwa  wakivaa sare  za kazi,  Kamsi alisema   wanawatambua kwa vile  wanamfahamu kila mteja wao na siyo lazima wawe na sare ndiyo wawatambue.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles