30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Makaburi ya halaiki yenye maiti 6000 yagunduliwa

Bujumbura, Burundi

KAMISHENI ya Ukweli na Maridhiano ya Burundi imetangaza habari ya kugundua makaburi sita ya umati yenye maiti 6000 katika mkoa wa Karusi, mashariki mwa nchi.

Mwenyekiti wa kamisheni hiyo, Pierre Claver Ndayicariye aliwaambia waandishi wa habari kuwa, maiti 6,032 na maelfu ya risasi zimepatikana karibu na milima ya Bukirasazi mkoani Karusi na kwamba miwani, nguo na rosari zimetumika kutambua wahanga hao.

Kamisheni hiyo iliyoundwa mwaka 2014 kwa ajili ya kufuatia jinai zilizofanyika nchini humo tokeo mwaka 1885 hadi 2008, kufikia sasa imefanikiwa kugundua makaburi ya halaiki 4,000 yenye miili 142,000 ya wahanga wa jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu.

Makaburi ya umati yamekuwa yakigundulika katika maeneo kadhaa nchini Burundi suala ambalo linawatia wasi wasi mkubwa watetezi wa haki za binadamu wanaodai kuwa, mbali na kufuatiliwa jinai za kihistoria, jinai za sasa zinazofanywa na utawala wa Rais Pierre Nkurunziza zinapaswa kufuatiliwa pia.

Hii si mara ya kwanza kwa makaburi ya umati kugunduliwa nchini Burundi

Hii ni katika hali ambayo, serikali ya Bujumbura pamoja na mashirika waitifaki yasiyokuwa ya kiserikali nchini Burundi yamekuwa yakipinga ripoti za mashirika ya kutetea haki za binadamu kama Amnesty International na Human Rights Watch yanayodai kuwa, kungali kunashuhudiwa hali ya ukandamizaji na ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu nchini humo.

Hali ya machafuko iliigubika Burundi tangu mwezi Aprili mwaka uliopita baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuteuliwa na chama chake cha CNDD-FDD kuwania tena urais kwa mara ya tatu.

Hata hivyo chama hicho hivi karibuni kilimteua Katibu Mkuu wa chama hicho, Evariste Ndayishimiye kuwa mgombea wa kiti cha urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles