25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Majizzo akumbuka tabasamu la Lulu akiwa jela

Bethsheba Wambura, Dar es SalaamMchumba wa muigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu, Francis Siza maarufu (Majizzo), ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram akikumbushia  siku ambayo alikwenda jela kumtembelea mpenzi wake huyo.

Majizzo ametuma ujumbe huo leo Jumanne Novemba 20, akiambatanisha na picha inayowaonesha wawili hao wakiwa katika ‘pozi’ la furaha baada ya sherehe ya kutoa mahari kwa Lulu iliyofanyika siku Jumapili iliyopita, Novemba 18, mwaka huu.

Katika ujumbe wake wa leo, Majizzo ameelezea namna alivyokuwa akipanga foleni kwenda katika gereza la Segerea kumuona Lulu aliyehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba 13, mwaka jana baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzie Steven Kanumba.

“Siku kama ya leo, muda kama huu nilikuwa kwenye foleni ya kuingia Segerea kumsalimia ‘Mrs Majizzo’, nilipofika ndani nilikutana na tabasamu kama hilo kwenye picha lakini kwa mapenzi ya Mungu leo imebaki kama kumbukumbu,” ameandika Majizzo.

Aidha kabla ya Majizzo kutuma ujumbe huo Lulu nae alituma ujumbe jana ambapo aliweka picha kama aliyotumia mchumba wake na kisha kuambatanisha na maneno yaliyosomeka ‘road to Franclizzy’ akimaanisha kuelekea katika siku maalumu ya Francis na yeye Elizabeth au Lizzy.

Ikumbukwe kuwa Septemba 30 mwaka huu Lulu alifanyiwa  ‘Surprise’ ya kuvalishwa pete ya uchumba katika sherehe za kipaimara ya mdogo wake na watoto wa Majizzo kitu ambacho kilimshtua yeye na mashabiki zake hadi kufikia wengine kusema ndoa ya wawili hao imekaribia.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,407FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles