23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

Majimbo matatu yawavuruga Ukawa

kahangwaNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

MAJIMBO matatu yameonekana kuvivuruga vyama vinavyonda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutokana na vyama hivyo kushindwa kusimamisha mgombea mmoja kama yalivyo makubaliano yao.

Kutokana na hali hiyo, vyama hivyo vimejikuta vikisimamisha wagombea wawili katika jimbo moja na hivyo kuzua utata katika majimbo hayo.

Majimbo yaliyoleta mvutano katika umoja huo ni Jimbo la Serengeti mkoani Mara, Mtwara Mjini mkoani Mtwara na Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. George Kahangwa, alisema hadi sasa umoja huo umefanikiwa kugawa majimbo yao kwa kufuata vigezo kwa asilimia 90 ya majimbo 265 ya Tanzania.

Alisema Jimbo la Serengeti linawagombea wawili kutoka katika vyama hivyo ambao ni Katibu Mkuu wa NCCR –Mageuzi, Mosena Nyambabe na Marwa Ryoba wa Chadema.

Jimbo jingine ni Mwanga lililopo mkoani Kilimanjaro ambako NCCR-Mageuzi imemsimamisha Youngsaviour  Msuya wakati Chadema imemsimamisha Henry Kilewo.

Jingine ni Mtwara Mjini, ambapo siku moja baada ya mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji kumtangaza mgombea wa CUF, Maftaha Nachuma kuwa mgombea wa Ukawa katika jimbo hilo, badala ya Hassan Uledi (NCCR- Mageuzi), umoja huo umeeleza kwamba tatizo la jimbo hilo halijapatiwa ufumbuzi.

Umoja huo unaoundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha NLD na Chama Cha Wananchi (CUF) jana ulitoa orodha ya majina ya wagombea ubunge watakaopeperusha bendera ya umoja huo nchi nzima.

Kwa upande wa majimbo ya Dar es Salaam majimbo mawili yalikuwa bado yapo katika mvutano kwa vyama vya CUF na Chadema ambayo ni Jimbo la Kigamboni na Segerea.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, majimbo hayo hivi sasa yamepatiwa ufumbuzi.

Wagombea 10 wa Dar es Salaam waliopitishwa kwa Chadema na majimbo yao katika mabano ni Saed Kubenea (Ubungo), Halima Mdee (Kawe), Mwita Waitara (Ukonga), Muslim Hassanali (Ilala), Lucy Magereli (Kigamboni) na John Mnyika (Kibamba).

Wagombea wa CUF, walioachiwa kwa Dar es Salaam ni Maulidi Said(Kinondoni), Julius Mtatiro (Segerea), Abdallah Mtolea (Temeke) na Kondo Bungo (Mbagala) .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles