Majeruhi watatu ajali ya lori la mafuta waruhusiwa

0
751

Aveline Kitomary, Dar es Salaam

Majeruhi watatu wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wameruhusiwa baada ya hali zao kiafya kuonekana ni nzuri.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 12, Daktari bingwa wa upasuaji wa Muhimbili,  Edwin Mrema amesema hali za wagonjwa wengine wanane waliobaki zinaendelea vizuri.

“Majeruhi walikuwa wamebaki 11 hivyo sasa wamebaki wanane kati ya 47 waliofikishwa Muhimbili Agosti 11, ambapo majeruhi 36 walipoteza maisha.

“Tunaendelea kuwatibu majeruhi na kuwatafuta wanasaikolojia na pia kuangalia kati ya wawili waliobaki wenye hali nzuri tutawaruhusu, kwahiyo leo hadi jioni tutawaruhusu majeruhi watatu,” amesema Dk Mrema.

Amewataja wagonjwa walioruhusiwa kuwa ni Mikidadi Issa na Shaban Omary na mwingine ambaye hakutajwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here