33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAJERUHI LUCKY VINCENT WAANZA KUOGA WENYEWE

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA

MAJERUHI watatu wa ajali ya basi la Shule ya Lucky Vincent, waliopo nchini Marekani kwa matibabu, wameanza kujihudumia wenyewe ikiwamo kuoga.

Majeruhi hao, Doreen Mshana, Sadia Awadh na Wilson Tarimo, walipata ajali Mei 6, mwaka huu wilayani Karatu huku wanafunzi wenzao 33, walimu wawili na dereva wakipoteza maisha.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) na Mwenyekiti mwenza wa Shirika la STEMM, Lazaro Nyalandu, alisema kuwa madaktari wamejiridhisha kuhusu maendeleo ya kupona kwa mifupa ya watoto hao.

Alisema Sadia na Wilson walipelekwa Kituo cha CNOS (Center for Neurosurgery Orthopedics and Spine) Jimbo la Dakota Kusini, ambako madaktari walijiridhisha na maendeleo ya kupona kwa mifupa, hivyo wakawatoa bandeji ngumu.

“Sadia na Wilson wameondolewa ‘Cast’ walizokuwa wamewekewa na sasa wanaweza kujiogesha wenyewe kwa mara ya kwanza tangu wafikishwe hospitalini,” alisema Nyalandu.

Kwa upande wake, Muuguzi wa Hospitali ya Mount Meru, Symphrosa Silali aliyeongozana na majeruhi hao, alisema Doreen aliyefanyiwa upasuaji katika uti wa mgongo, afya yake inaendelea kuimarika.

“Jumatatu wiki hii alitolewa pini kwenye mkono wa kushoto, lakini pia ameweza kuchezesha mguu wake wa kulia hatua inayoonyesha matumaini katika uponaji wake,” alisema muuguzi huyo kupitia ukurasa wa Facebook wa Nyalandu.

“Watoto wote wanafanya mazoezi mara tatu kwa wiki, wapo wataalamu pia wanaowafanyia mazoezi ya namna gani wanaweza kukabiliana na vitu vilivyokuwa mbele yao ili waweze kuvisahau.

“Lakini pia kuna mazoezi ya viungo yanayowezesha viungo vyao kuendelea kuzoea kutumia mikono, miguu yao. Lakini pia wanafundishwa kufanya vitu vidogo vidogo wenyewe kama kupiga mswaki, kuoga na kuvaa nguo.

“Jumatano watoto wote wametolewa ‘mihogo’ na wanaendelea vizuri, hatua ambayo imewawezesha kutumia viwiko vya mikono vizuri, ikiwamo kuendelea na kufundishwa namna ya kukunja mikono na kuinyoosha,” alisema Silali na kuongeza:

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles