27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

MAJASUSI MAREKANI KUTOA USHAHIDI BUNGENI

Washighton, Marekani


WAKUU wa mashirika mawili makuu ya ujasusi ya Marekani wanatarajiwa kutoa ushahidi kwa kamati za Bunge la Congress kuhusu madai kwamba Urusi iliingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka jana.

Pia, watatoa ushahidi kuhusu tuhuma kwamba kulikuwa na ushirikiano na mawasiliano kati ya Urusi na maafisa wa kampeni wa Rais Donald Trump.

Kadhalika, wataangazia tuhuma zilizotolewa na Trump kwamba simu zake zilidukuliwa na mtangulizi wake Barack Obama.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uchunguzi wa Jinai la FBI, James Comey na Mkuu wa Idara ya Taifa ya Usalama, Mike Rogers watatoa ushahidi katika kikao nadra sana cha wazi cha kamati ya Bunge kuhusu ujasusi.

Trump ametaja uchunguzi huo kuwa usio wa haki.

Urusi imekanusha tuhuma kwamba ilijaribu kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles