27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Majangili wafungwa miaka 120

Na Nathaniel Limu, Singida

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi mkoani Singida, imewahukumu washtakiwa sita  adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka 120 na kulipa faini  ya Sh bilioni 1.4, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la   kukutwa na vipande 53 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh milioni 149.336 na kosa la jingine la uwindaji haramu.

Washtakiwa hao, ni Eliud Selema Mayunga (38) mkazi wa Kijiji cha Kiomboi, Ramadhani Said, (47) mkazi wa Itigi na Leonard  Sunzu (31), mkazi wa Kijiji cha  Karangari.

Wengine ni Philemon Kanyonga (31), mkazi wa Kitaraka Itigi, Iddi Waziri, Issah Ustadh (30) mkazi wa Kijiji cha Kiomboi na Jimmy Charles (39) mfanyabiashara wa Tabora Kyombo.

Mwendesha mashtaka na Mwanasheria wa Serikali, Petrida Mutta alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Jocye Minde kuwa Machi 31, mwaka 2014 muda usiojulikana, washtakiwa kwa pamoja walikamatwa wakiwa wamehifadhi na kumiliki vipande vya meno 53 vya meno ya tembo nyumbani kwa mshtakiwa Issa Ustadh, huku wakijua wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, aliiomba mahakama hiyo kuwapa washtakiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwao.

“Mheshimiwa mpaka sasa tunaendelea kusikia na kuona vitendo vya uwindaji na biashara za nyara za Serikali vikiendelea kushamiri.Vitendo hivi haviwezi  kufumbiwa macho, kwa sababu fahari ya nchi hii ya wanyama pori, itatoweka.

“Kwa hiyo naiomba mahakama yako itoe adhabu kali, si tu iwe fundisho kwa washtakiwa, bali iweze kuogofya na watu wengine wanaotarajia kujihusisha na uwindaji na biashara haramu ya nyara za Serikali,”alisema.

Kwa upande wa washtakiwa ambao wakili wao, Josephat Raphael hakuwapo wakati hukumu hiyo inatolewa, kila mmoja kwa nafasi yake, aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu.

Akitoa hukumu hiyo, ambayo ilishuhudiwa na  umati wa wasikilizaji, Hakimu Minde alisema upande wa Jamhuri umethibitisha bila kuacha shaka kwamba washtakiwa wanayo hatia kwa makosa yote mawili.

“Kwa kosa la kwanza la kumiliki kinyume na sheria  vipande 53 vya meno ya tembo, kila mmoja wenu atatumikia jela miaka 20 na kila mmoja wenu, atalipa  faini ya Sh 248,893,333.30  kwa kosa la pili la kujihusisha na uwindaji haramu, kila mmoja wenu”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles