25.9 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

MAJAMBAZI WAVAMIA KIJIJI, WAPORA FEDHA

Na WALTER MGULUCHUMA-KATAVI

WATU watano wanaosadikiwa kuwa ni  majambazi, wamevamia Kijiji cha Itenka, Tarafa ya Nsimbo wilayani Mpanda mkoani Katavi na kuwapora Sh milioni 4, baadhi ya wafanyabiashara wa maduka katika kijiji hicho.

Wakati wa tukio hilo lililotokea jana, majambazi hao walitishia kuwalipua kwa baruti wafanyabiashara hao na kusababisha wakimbie na kutelekeza maduka yao.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Katavi, Benedict Mapujila, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa moja na nusu usiku kijijini hapo.

Alisema kwamba, siku ya tukio majambazi  hao wapatao watano walifika kijijini hapo na kuwavamia wafanyabiashara kwa kulipua  baruti hewani na kusababisha watu wakimbie na kuacha maduka wazi.

“Baada ya wafanyabiashara hao kukimbia na kuacha wazi maduka yao, majambazi hao waliingia ndani ya maduka mawili na kupora Sh milioni nne na kutokomea kusikojulikana.

“Baadaye wananchi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi juu ya tukio hilo na polisi walifika  eneo hilo baada ya muda mfupi, lakini hawakufanikiwa kuwakamata.

“Kisha polisi walifanya uchunguzi lakini hawakufanikiwa kuona ganda lolote la risasi, hali iliyoonyesha walitumia baruti kuwatishia wafanyabiashara.

“Hata hivyo, hadi sasa hakuna mtu yeyote ambaye amekamatwa kuhusiana na tukio hilo ingawa msako wa kuwasaka watu hao unaendelea,” alisema kaimu kamanda huyo wa polisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles