25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAJAMBAZI WAPORA MILIONI 22/- , VOCHA SIKU YA PASAKA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Khamis Issa

 

Na MURUGWA THOMAS,

WATU wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia duka na  kupora   Sh  milioni 22  na vocha  za simu za mitandao tofauti zenye thamani ya Sh milioni 47 mali ya mfanyabiashara Revocatus Zunza  wa mjini Tabora.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Khamis Issa alisema  tayari polisi wanafanya  uchunguzi wa kina  kubaini waliohusika na uvamizi huo ikiwa ni pamoja na kuwatia mbaroni.  

Tukio hilo linadaiwa kutokea Aprili 16, mwaka huu katika mtaa wa Jamhuri katikati ya mji wa Tabora   siku ya Sikukuu ya Pasaka   wakati mmiliki wa duka hilo akiwa kwenye mapumziko ya Pasaka.

Duka lililovunjwa na kuibwa lipo   mkabala na ilipo sanamu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu   Nyerere eneo la soko kuu la mjini Tabora jengo ambalo linamilikiwa na familia ya marehemu Dk.  Othman.

Mmiliki wa duka hilo, Revocatus Zunza ambaye ni wakala wa kuuza vocha za jumla wa makampuni mbalimbali ya simu za mkononi, alisema aligundua wizi huo Jumatatu asubuhi alipofika kufungua duka.  

Zunza alidai  watu waliohusika na wizi huo inaonekana waliingia ndani ya duka lake kupitia chumba cha jirani ambacho kilivunjwa tofali za moja la ukuta wake na kuiba fedha  na vocha.

“Siku ya tukio nilipita eneo hili nikitokea kanisani, nilikuta mlango wa chumba cha jirani ambacho mpangaji wake hatujawahi kuonana ukiwa wazi.

“Nje kulikuwa na mmiliki wa jengo   na watu ambao walionekana kufanya ukarabati, sikutilia shaka nadhani inatia shaka,” alisema.

Baadhi ya watu wanaofanya biashara jirani na eneo la tukio wamedai kuwa Jumamosi ya Aprili 15, mwaka huu waliwaona watu wakifungua mlango wa chumba hicho.

Walisema watu hao waliingiza ndani mitungi ya gesi kitendo hicho hakikuwashutua kwa vile  wananchi wengi hufanyia shughuli zao hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles