28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: Wananchi washirikishwe kwenye ujenzi wa miundombinu

Anna Potinus

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesisitiza wananchi kushirikishwa katika utekelezaji wa miradi ya ukarabati na ujenzi wa miundombini kupitia makundoi madogo madogo kwa lengo la kuwasaidia kuongeza kipato chao na kujikwamua na umasikini.

Ametoa rai hiyo leo Jumamosi Julai 20, alipokua akizungumza na wananchi katika uzindinduzi wa safari mpya ya treni ya mizigo ya Tanga – Kilimanjaro yenye jumla ya kilomita 353, ambapo ameagiza vibarua walioshughulika katika ujenzi wa reli hiyo kupewa ajira za kudumu ili waweze kujikimu kimaisha.

“Kama ilivyokuwa mradi wa standard gauge, njia ya reli ya Tanga mpaka Moshi ukarabati wake umetekelezwa na wazawa ukihusisha vijana wetu ambao wako hapa hivyo wabadilishwe na kuwa watumishi wa kudumu ili waweze kujikimu kimaisha,” amesema.

“Ni matarajio yangu kupata taarifa kuwa ajira zao zimekamilika ili waendelee kuitunza na kuikarabati reli hii na watakuwa watumishi wema watakaohakikisha reli inafanya kazi siku zote bila ya mtu yoyote kudokoa chuma wala boriti mahali palipowekwa vifaa,” amesema.

Aidha Majaliwa ameaasa wananchi wote wa Mkoa huo kuhakikisha wanalinda na kutunza miundombinu hiyo na kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake ambapo ameagiza kufanyika kwa utaratibu utakaoruhusu wananchi hao kujishugulisha na ujasiriliamali katika eneo hilo ili waweze kunufaika,” amesema.

“Mkuu wa kituo cha hapa andaa utaratibu wa wajasiriliamali kuja kufanya biashara hapa, mama lishe, wabeba mizigo na wengine muwaongoze na kutoa elimu ili waanze kunufaika na mkitoka hapa andaeni matangazo ili watu waanze kuja na shughuli hiyo ianze mara moja,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles