24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA: WALIOKULA MALI ZA LUPEMBE KUSAKWA

Na Mwandishi Wetu, Njombe


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Serikali itahakikisha inawasaka watu wote waliohusika na upotevu wa mali za Kiwanda cha chai cha Lupembe na kuwachukulia hatua.

Amesema pia Serikali haitoipa nafasi migogoro yote ya uwekezaji inayosababisha wananchi kutopata ajira, bali itatatuliwa bila ya kusimamisha uzalishali.

Pia amewataka wawekezaji waliomilikishwa viwanda, wahakikishe wanafuata kanuni na sheria ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na wananchi waweze kupata tija.

Waziri Mkuu, alitoa kauli hiyo juzi, wakati alipotembelea Kiwanda cha Lupembe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Njombe.

Mali za kiwanda hicho, vikiwamo vipuri na vyombo vya usafiri; malori na magari madogo 17 vilipotea, baada ya Ushirika wa Wakulima wa Chai Muvyulu kuvamia kiwanda.

Kiwanda hicho kinakabiliwa na mgogoro kati ya mwekezaji, Lupembe Tea Estate na Ushirika wa Wakulima wa Chai Muvyulu ambao Waziri Mkuu ameahidi kuutafutia ufumbuzi.                               

“Migogoro yote inayosababisha watu kutopata ajira, haitapewa nafasi. Tutaisikiliza na kuipatia ufumbuzi bila ya kusimamisha uzalishaji.

“Ushirika uliyumba na umekuwa ukiharibiwa na waliopewa dhamana, ndiyo sababu tuliamua kuufumua uongozi kuanzia juu na tutashuka hadi chini,” alisema.

Alisema Serikali itahakikisha mwenye haki anapata haki yake na haitakubali kuona kiwanda hicho kikisimamisha uzalishaji. Pia inafuatilia kujua mwekezaji huyo alipataje kiwanda.

“Lupembe ni miongoni mwa viwanda ambavyo vilikufa, sasa kimeanza uzalishaji, hatutakubali kife kutokana na migogoro ya wanaushirika na mwekezaji. Kiwanda hakitasimama ng’o.

“Hatuwezi kukubali migogoro iendelee kwani haina tija, inaumiza wananchi. Najua ushirika ni wa wakulima, tunataka uwe imara, hatutaki ushirika wenye mizengwe mizengwe,” alisema.

Katika hatua nyingine, Majaliwa amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kufanya uchunguzi katika kiwanda hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles