24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Majaliwa: Wakuu wa mikoa igeni Ruvuma

Na Mwandishi Wetu -Songea

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka wakuu wa mikoa mingine kuiga mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme wa kuweka makongamano ya uwekezaji ili kupanua fursa za uwekezaji na  uanzishwaji wa viwanda.

 Wito huo aliutoa hivi karibuni, wakati akizindua kongamano la viwanda na uwekezaji, lililohudhuriwa na wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali ndani ya nchi.

Majaliwa alisema kazi ya kuwavuta wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali, ni jukumu la maeneo husika kutangaza fursa zilizopo.

“Tumeamua kuridhia uwekezaji huo ili kuenda sambamba na kaulimbiu ya Serikali ya viwanda, yaani uchumi wa kati,” alisema.

Majaliwa alisema Serikali imejitahidi kuweka miundombinu mbalimbali, ikiwamo ya umeme, barabara pamoja na ardhi ya kutosha yenye rutuba  nzuri  ambayo kila zao linakubali kwa wanaohitaji kuwekeza katika sekta  ya kilimo.

 Alisema mkoa huo una madini ya aina mbalimbali, ikiwemo dhahabu na makaa ya mawe,  hivyo hakuna mwekezaji atakayeshindwa kuwekeza.

Naye Mndeme akielezea uwekezaji uliopo, alisema wamejipanga kikamilifu katika hlmashauri za wilaya  zilizopo kuwekeza.

Alisema ardhi iliyopo hadi sasa mkoani humo ni hekta milioni 47, ambayo inaweza ikafaa katika uwekezaji na maeneo yake yanafikika kutokana na miundombinu iliyopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles