25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: Viongozi simamieni elimu kwa watoto wa kike

Mwandishi wetu

Wakuu wa mikoa na wilaya nchini wameaswa kusimamia ipasavyo suala la elimu hususani kwa watoto wa kike na kuchukua hatua kwa watakaowakatisha masomo.


Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo cha mafunzo ya Amali cha Daya kilichopo Mtambwe Wilaya ya Wete, Kaskazini Pemba.


Amesema serikali imedhamiria kuwalinda watoto wa kike lengo likiwa ni kuhakikisha wanamaliza masomo yao na hatimaye waweze kujikwamua wao pamoja na familia zao.


Ameongeza kuwa watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa na jamii kwa kuachwa waendelee na masomo yao bila ya usumbufu wowote na kwamba atakayebainika kukatisha masomo yao adhabu yake ni miaka 30 jela.


“Wanafunzi wa kike hakikisheni mtu yeyote atakayekugusa au kukufuatilia nenda kamshtaki kwa kiongozi wa kijiji husika, na nyie vijana jihadharini na watoto wa shule ukikutwa naye utakwenda jela miaka 30,” amesema Waziri Majaliwa.


Awali, akisoma taarifa za ujenzi wa chuo hicho, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Madina Abdallah amesema mpaka kukamilika kwa mradi huo utagharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 25.8 ambapo Dola milioni 23.4 zimetolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika huku Dola milioni 2.4 zikitolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles