23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: tutahakikisha wananchi wote wanapata maji

                         Bethsheba Wambura  

Serikali imesema itahakikisha huduma ya maji safi na salama inapatikana katika vijiji vyote nchini na tatizo la maji linakwisha kabisa.

Serikali imetoa agizo hilo jana jioni Alhamisi Novemba Mosi kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mponde jimbo la Bumbuli, Lushoto.

Waziri Mkuu ambaye jana alihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga, aliwapongeza wakazi wa wilaya ya Lushoto kwa kutunza mazingira na vyanzo vya maji, serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote yenye changamoto hiyo nchini.

“Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dk. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama na hiki ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali hivyo nawaomba wananchi muendelee kutuamini, ” alisema.

Naye Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alisema Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi, ukarabati wa miradi ya maji, ambapo mkoa wa Tanga umetengewa Sh. bilioni 13.

Aweso alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa wakandarasi wanaojenga miradi ya maji wazingatie viwango vya ubora kwa kuwa Serikali inatumia fedha nyingi katika kugharamia miradi hiyo.

“Serikali inatoa fedha kwa ajili ya miradi ya maji alafu mnazitumia kujengea majumba na kununua magari, safari hii mtazitapika tunataka miradi itekelezwe kwa kuzingatia viwango, naahidi kufuatilia kwa kina ujenzi wa miradi yote ya maji nchini ili kuhakikisha kama inalingana na thamani halisi ya fedha zinazotolewa katika miradi hiyo,” alisema Aweso.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles