26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

Majaliwa mgeni rasmi wiki ya nenda kwa usalama barabarani Mwanza

Na Clara Matimo, Mwanza

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yatakayofanyika kitaifa mkoani Mwanza katika uwanja wa furahisha uliopo Wilaya ya Ilemela yakiongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Tanzania bila ajali inawezekana – Timiza wajibu wako’.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Ramadhan Ng’anzi, akielezea jinsi maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani mwaka 2023 yatakavyofanyika.

Akitoa taarifa kwa vyomba vya habari leo Machi 13, 2023 kuhusu maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima amesema takwimu nyingi za ajali za barabarani mkoani humo zinasababishwa na mwendo kasi, ubovu wa vyombo vya moto, baadhi ya madereva kuendesha wakiwa wamelewa, kujaza abiria na mizigo kupita kiasi, kupita gari la mbele bila kuchukua tahadhari na kuegesha magari mabovu yaliyoharibika barabarani kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Malima takwimu za ajali za barabarani mkoani humo kwa kipindi cha Januari hadi Desemba, 2022 jumla ya ajali kubwa 81 zimeripotiwa, zilizosababisha vifo vya watu 71 na majeruhi 96, ajali kubwa za pikipiki ni 30 zilizosababisha vifo vya watu 25 na kujeruhi 26 ambapo amesema hali hiyo si nzuri na kuwataka watumiaji wote wa barabara kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.

“Hatuwezi kuvumilia wananchi wapoteze maisha na wengine kupata majeraha ama ulemavu wa kudumu kutokana na ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva wazembe, ili kukabiliana na hali hiyo Mkoa wa Mwanza tumejipanga kupunguza ajali hizo kwa kuchukua hatua na kuweka mikakati mbalimbali ikiwamo kukagua vyomba vya moto mara kwa mara, kuwahamasisha bodaboda kufuata alama na ishara zinazotolewa na wasimamizi wa sheria na kutoegesha magari mabovu barabarani zaidi ya masaa mawili.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na kamati ya usalama barabarani ya mkoa wa Mwanza pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima(hayupo pichani) akielezea kuhusu maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani itakayofanyika kitaifa mkoani humo.

“Tumeweka kauli mbiu ya kudumu kuhusu usalama barabarani inayosema ‘Karibu Mkoa wa Mwanza ;Tafadhari zingatia sheria na Kanuni za Usalama Barabarani, Epuka Adhabu Kali’, ili kuepuka adhabu kali natoa wito kwa watumiaji wote wa barabara katika Mkoa wa Mwanza hasa madereva kuzinagtia udereva wa kujihami kuepuka mwendo kasi, kuyapita magari mengine sehemu ambayo ni salama na kuchukua tahadhari kubwa wanapopita kwenye mteremko, kona, eneo la makazi na kwenye hifadhi za wanyama,”amesema Malima.

Pia, amewataka abiria kutoshabikia vitendo vya ukiukwaji wa sheria ikiwamo mwendokasi bali wakemee na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wanapoona ukiukwaji huo pamoja na bodaboda kuacha tabia ya kupakia abiria zaidi ya mmoja na kuzingatia uvaaji wa kofia ngumu.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Ramadhan Ng’anzi amesema lengo kuu la maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ni kuendelea kutoa elimu ya sheria, kanuni na taratibu za Usalama Barabarani kwa makundi yote ya watumiaji wa barabara.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Jana niisafiri kwa Bajaji kutoka Mesaki hadi Kariakoo. Pale Aga Khani tukashuhudua maaskari wakiwakamata waendesha Bajaji na Bodaaboda na kuwasomba
    Nikamuuliza dereva wangu naye akanaieleza huo ni mradi wa wakubwa. watapelekwa central kisha watatozwa fedha bila risiti. Eti kosa lao ni kuingia maeneo ya jijini bila ya ruhusa !!! DU
    Hii kamati inajua haya au inapoteza fedha tu kwa masemina yasiyo na tija?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,405FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles