27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa kuwasili Mwanza kesho

Na Clara Matimo, Mwanza

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kuwasili mkoani Mwanza Oktoba 15, 2022 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne mkoani humo.

Hayo yamebainishwa Oktoba 13, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima wakati akitoa taarifa ya ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa kwa waandishi wa habari ambapo alieleza kwamba akiwa mkoani humo atakagua ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzindua jengo la huduma ya macho lililojengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando (BMC).

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima akiwapa taarifa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusu ujio wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani humo kwa ajili ya ziara ya siku nne ya kikazi.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa atawasili kesho Oktoba 15  saa10 jioni kuanza ziara ya kikazi mkoani hapa ambapo ataendelea na majukumu ya kikazi  hadi Oktoba 18, 2022.

“Oktoba 16, 2022 asubuhi atakagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Magufuli kisha atawasalimia wananchi wa Busisi na usagara baada ya hapo ataelekea Bukwimba Wilayani Kwimba kukagua maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) halafu ataelekea hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando kuzindua jengo la huduma ya macho,”amesema Malima na kuongeza:

“Oktoba 17, 2022 asubuhi ataenda Wilayani Ukerewe kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Irugwa na ujenzi wa shule ya sekondari Irugwa vinavyojengwa katika kisiwa cha Irugwa kisha ataenda kisiwa cha Gana kukagua ujenzi wa zahanati ya Gana iliyopo hatua ya msingi,” amesema Malima.

Kwa mujibu wa Malima baada ya kutoka Ukerewe siku hiyo ya Okotoba 17, saa tisa alasiri Waziri Mkuu Majaliwa atakagua maendeleo ya ujezi wa stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ya Nyegezi kisha atawasalimia wananchi wa eneo hilo.

“Baada ya kuwasalimia wananchi Mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa ataenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa Meli ya MV Mwanza Hapa Kazi tu ambao unaendeleo kwenye bandari ya Mwanza Kusini.

“Wito wangu kwa wananchi wote wa mkoa wa Mwanza kama ilivyo jadi yetu kuwakarimu wageni wajitokeze kwa wingi katika maeneo yote ambayo  Mheshimiwa Waziri Mkuu atafanya ziara kwa ajili ya kumpokea kiongozi wetu,”amesisitiza Majaliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles