27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Majaliwa kufungua mkutano wa Azaki leo

Ramadhan Hassan-Dodoma

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Wiki ya Azaki leo jijini hapa, ambao unatarajia kushirikisha zaidi ya asasi za kiraia 500 kutoka Tanzania Bara na visiwani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS), Francis Kiwanga, alisema lengo la kongamano hilo ni kuimarisha ubia kati ya asasi za kiraia na wadau mbalimbali katika juhudi za kutimiza azma ya kuiletea Tanzania maendeleo.

Kiwanga alisema kupitia kongamano hilo, asasi za kiraia zitafanya majadiliano ya kina kuhusu kazi zao, kubadilisha uzoefu na kuona jinsi ambavyo zinaweza kushirikiana zenyewe kwa zenyewe na wananchi, Serikali, Bunge, wabia wa maendeleo na sekta binafsi.

“Kaulimbiu ya wiki hii ni ‘ubia kwa maendeleo ushirikiano kama chachu ya maendeleo’. 

“Kauli hii inaweka msisitizo kwenye dhana nzima ya ushirikiano ili nchi ifanikishe dira yake ya maendeleo na kufikia kiwango cha kukua kimaendeleo kama ilivyoazimiwa ndani ya mpango wake wa maendeleo endelevu, ushiriano kati ya wadau mbalimbali wa maendeleo, ndilo tumaini kuu la kutimiza azma hiyo,” alisema.

Alisema asasi hizo zitatoka sekta ya kilimo, watoto, afya, vijana, watu wenye ulemavu, elimu na nyinginezo, wataonyesha shughuli zao kwa wadau wakiwemo wananchi,” alisema Kiwanga.

Alisema FCS itatoa tuzo za umahiri wa asasi za kiraia ili kusherehekea na kutambua  ufanisi na michango ya taasisi na watu binafsi, ambao kwa namna moja au nyingine wamechochea uimarishaji na utekelezaji wa sera za maendeleo nchini.

“Zaidi ya asasi za kiraia 15 zilizoshirikiana na FCS kuandaa Wiki ya Azaki zitahakikisha zinashiriki, ikiwemo Legal Human Rights Centre (LHRC), Legal Services Facilities (LSF), Save the Children, Wajibu Institute, Un Women, Oxfam, Twaweza Policy Forum, Msichana Intiative, Hakirasilimali na United Nations Associations of Tanzania (UNA).

“Nyingine ni Tanzania Accountability Tanzania (Ac T2), Sikika, Tanganyika Law Society (TLS), Shirika la Walemavu Tanzania (Shivyawata) na Tanzania Association of Non Gavemment Organization (Tango),” alisema. 

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Womap, Fatma Tawfiq alisema;“Umma utoe dhana potofu kwamba asasi za kiraia zipo kwa ajili ya kupata pesa, wanatakiwa kutambua kuwa zipo kwa malengo ya kusaidia jamii na siyo kujitajirisha wenyewe fedha.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles