25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa awataka Watanzania kukua kiuchumi kwa kuchangamkia fursa za mikopo

Na Mwandishin Wetu, Mtanzania Digital

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kukua kiuchumi kwa kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na Taasisi za fedha zikiwemo Benki.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Tanzania Commercial Bank, alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, yaliyofanyika Desemba 18,2023 jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo alipotembelea Banda la Tanzania Commercial Bank katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, na Wiki ya Ustawi wa Jamii, iliyoenda sambamba na uzinduzi wa vipindi vya Malezi, Makuzi na maadili kwa vijana, iliyofanyika Desemba 19,2023 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Aidha, Majaliwa alisema kutokana na changamoto za kiuchumi familia nyingi zinashindwa kupata muda wa kutosha kulea watoto na vijana ambao ni muhimu katika ujenzi wa Taifa la sasa na baadaye, hivyo mada hiyo ni kengele ya amshaamsha kwa kila mtendaji na mwanajamii kutambua kuwa suala la malezi na makuzi ya watoto na vijana ni msingi wa maendeleo ya Taifa letu.

Katika tukio hilo, Tanzania Commercial Bank walishiriki wakiwa ni wadhamini wa maadhimisho hayo.

Hatua hiyo ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya kuhakikisha makundi mbalimbali ya kijamii yanaendelea kunufaika kiuchumi, nakwamba Tanzania Commercial Bank imeendelea kuwa mdau mkubwa kwa kuweka mazingira wezeshi yakiwamo huduma za mikopo itakayosaidia kuchochea maendeleo ya wanawake, makundi mbalimbali na watanzania wote nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles