26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa awataka wanaoishi mabondeni  kuhama

Kassim (1)WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewatahadharisha wananchi wanaoishi mabondeni kuhama mara moja huku akiwataka viongozi wa serikali za vijiji na wilaya kuwasaidia  kuwahamisha   wanaoishi maeneo hatarishi.

Pia amesema kwa  sasa kitengo cha maafa kinaboreshwa  kiwe wakala wa kuratibu shughuli zote za maafa katika maeneo yote nchini ili kutoa huduma kwa wakati   zinapojitokeza.

Alisema tayari yameanza mazungunzo ndani ya serikali ili kituo hicho kiwe kama wakala ambao utakuwa unaratibu shughuli zote za maafa popote na na   kitatengewa fedha kutafuta maturubai, vibanda vya kujihifadhi kwa muda mfupi, dawa na kununua chakula   na mahitaji mengine.

“Ili inapotokea maafa kitengo chetu kifike mara moja na kuanza kutoa huduma kwa wananchi lakini kwa sasa tumejiimarisha vizuri maeneo yote yenye maafa wameshayapitia na wataalamu wetu wapo huko kwenye maafa kunusuru maisha ya watanzania wenzetu kulingana na mvua nyingi iliyonyesha,” alisema Majaliwa.

Majaliwa aliyasema hayo  bungeni jana wakati  akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalamu, Mariam Kisangi (CCM), ambaye alisema kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa mvua inanyesha bila kueleweka na imeua mazao mengi katika maeneo mbalimbali hali ambayo inaonyesha kuna viashiria vya njaa.

“Je serikali yetu imejipanga vipi katika kukabiliana na janga kubwa la njaa ambalo linaweza kuja baadaye kutokana na mbadiliko ya hali ya hewa,” alihoji Kisangi.

Akijibu swali hilo, Majaliwa alisema serikali imejipanga kuwahudumia watanzania ambao wamepata madhara na mpango huo upo kwenye ofisi yake kupitia kitengo cha maafa, hivyo   tathimini inaendelea kufanyika.

Majaliwa alisema tathimini hiyo inafanywa na halmashauri kupitia kamati   za maafa katika maeneo yao na baada ya kumaliza taarifa itapelekwa kwa mkoa kwa ajili ya kufanya mapitio na ofisi yake kutoa msaada  kadiri walivyoomba katika maeneo yao.

Majaliwa alisema pia kuwa kwa sasa kuna chakula cha kutosha na tayari kimeanza kupelekwa  katika maeneo yote yaliyopata maafa.

“Nataka nitoe wito tulime sana tupate chakula kingi tuweze kutunisha hifadhi yetu ya chakula ili tunapopata tatizo la uhitaji wa chakula basi chakula hicho kiweze kupelekwa maeneo yote yenye maafa,” alisema Majaliwa

Aliwataka wananchi ambao wapo katika maeneo hatarishi, wapishe maeneo hayo ili wasipate madhara kadiri mvua inayoendelea kunyesha nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles