31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa awataka viongozi vyama vya siasa kulinda amani

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuwa vinara katika kulinda amani na kukemea viashiria vya uvunjifu wa amani hasa wakati huu wa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Ametoa kauli hiyo leo Novemba 10,2024 wakati akifungua kongamano la umuhimu wa amani lililoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu wa Shia Tanzania (TMSC) kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Amani ikiwepo kila Mtanzania ataweza kujitokeza na kushiriki katika uchaguzi huu unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu, viongozi wa vyama vya siasa wawe vinara katika kulinda amani na kukemea viashiria vya uvunjifu wa amani,” amesema Majaliwa.

Pia ameipongeza jumuiya hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kulinda amani na kukemea maovu na maadili yanayokiuka utamadani wa Mtanzania.

Aidha amesema Serikali imeridhia ombi la jumuiya hiyo na kuwapa ardhi katika eneo la Msomera jijini Tanga kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha ufundi stadi na chuo cha kilimo na kwamba uwepo wa taasisi hiyo katika maeneo mbalimbali nchini utaongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo.

Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Shia Tanzania, Walema Nassoro, amesema wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha amani nyakati zote hasa wakati wa uchaguzi kwa kuandaa makongamano mbalimbali.

Ameishukuru Serikali kwa kuwapatia ardhi ambayo itasaidia kuongeza nguvu kazi na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles