27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA ATOA SOMO IDARA YA UHAMIAJI

Na AZIZA MASOUD

-KYELA
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Idara ya Uhamiaji kuhakikisha watu wanaoingia nchini kupitia mipaka iliyopo wanakidhi vigezo kabla ya kuwapa kibali cha ukimbizi kwa kuwa baadhi yao wanakimbia njaa katika nchi zao.

Majaliwa alitoa kauli hiyo katika mpaka wa Kasumulu alipokutana na watumishi wa taasisi na idara mbalimbali wakiwamo wa uhamiaji na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Alisema  idara  hiyo ya uhamiaji inapaswa kuwa makini na watu wanaoingia kutoka nchi jirani kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakitoa maelezo ya udanganyifu ili wapate kibali cha kuishi nchini kama wakimbizi.

“Idara ya Uhamiaji ina changamoto nyingi, hivi sasa  wananchi wanakuja nchini wanakimbia njaa wakija hapa wanasema nchini kwao kuna vita, idara ihakikishe inachuja watu hawa,”alisema Majaliwa.

Alisema kitendo cha wananchi wa nchi za jirani kuingia nchini bila utaratibu kinahatarisha ulinzi na usalama wa taifa.

Alisema kwa sasa limekuwapo wimbi la matumizi mabaya ya silaha ambazo wananchi hawana uzoefu nazo lakini zimekuwa zikitumika mitaani.

“Watu wanafanya uhalifu na silaha ambazo watanzania hawana uzoefu nazo kufanya uhalifu.

“Mfano nimepata taarifa kuna wahamiaji Wasomali wamekamatwa Kyela, watu hawa walipotoka mnapajua, uhamiaji muwe makini,”alisema Majaliwa.

Alisema idara hiyo pia inapaswa kuendelea kupanua wigo wa ulinzi na usalama katika mipaka yote nchini pamoja na kuimarisha utambuzi wa wananchi wanaoingia na kutoka.

Aliipongeza TRA kwa kufikia asilimia 100 miaka mitatu mfululizo na kuvuka malengo iliyojiwekea.

Awali , Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alisema idara ya uhamiaji imekamata wahamiaji haramu 87 ambao waliingia kupitia mipaka mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles