26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa atoa agizo kwa viongozi Ruvuma

MWANDISHI WETU-RUVUMA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ameutaka uongozi wa Mkoa wa Ruvuma uhakikishe kuwa vijana wote wanaomaliza darasa la saba kwenye kila halmashuri  za mkoa huo wanakwenda kuanza kidato cha kwanza.

Agizo hilo alilitoa jana wakati akizungumza na viongozi wa mkoa baada ya kuwasili uwanja ndege wa Songea kuanza ziara ya kikazi  ya siku nne.

Alisema halmashuri zote za mkoa huo zijikite katika kujenga madarasa ili wanafunzi wote waliofaulu ambao wanatakiwa kwenda sekondari waende.

“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuahakikisha kwamba watoto wote wenye sifa za kupata elimu ya seondari wanapata elimu hiyo kote nchini, hivyo juhudi za makusudi lazima zifanywe na kila halmashauri ili kutimiza azma,” alisema Majaliwa.

Akizungumzia suala la utoro shuleni, alisema hilo ni moja kati ya maeneo yanayozorotesha juhudi kubwa za Serikali za kuwapatia  watoto wa Tanzania elimu katika  maeneo mengi nchini na lazima viongozi wa wilaya na mikoa wasimame imara ili kukomesha hali hiyo.

Alisema viongozi wa ngazi zote katika mikoa na wilaya ndiyo hasa wanaoweza kumaliza tatizo la utoro wakishirikiana kwa karibu na wanavijiji ambao wanaishi na watoto hao na wanajua ni watoto  wangapi hawaendi shule.

Hivyo Waziri Mkuu aliwataka viongozi hao kutoa maelekezo na miongozo itakayowabana  watoto watoro  pamoja na wazazi au walezi wao kwani wanayo mamlaka  na uwezo wa kuchukuwa hatua  kwa mujibu wa sheria za nchi.

Akizungumzia  zao la korosho  aliwataka viongozi wa Mkoa wa Ruvuma kuwaondolea hofu wananchi wanaolima zao hilo katika mkoa huo kwa kuwahakikishia  kwamba Serikali inazo fedha za kutosha kununua korosho zote zilizovunwa na wakulima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles