26.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Majaliwa ataka elimu ya kupanga korosho kwa madaraja itolewe

Mwandishi wetu-Lindi


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amewaagiza warajisi wasaidizi wa ushirika katika mikoa yote inayolima korosho nchini, waandae semina kwa maofisa ushirika, viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS), maofisa ugani na wakulima  kuwawezesha kubaini na kupanga korosho katika madaraja kuanzia ngazi ya vyama vya msingi.

Alisema jambo hilo litasaidia mkulima aweze kujua korosho aliyoipeleka ina ubora gani akiwa huko kijijini na wanapoifikisha kwenye ghala kuu wafanye kazi ya kuthibitisha.

Hatua  hiyo itasaidia kuondoa malalamiko kuhusu madaraja, alisema .

“Hatua hii licha ya  kuthibitisha ubora itasaidia kuboresha uzalishaji kwa vile  wakulima wataelimishwa namna ya kuimarisha na kuboresha uzalishaji wa korosho nchini ikiwa ni pamoja na matumizi bora ya viatilifu,’’alisema.

Majaliwa alisema hayo jauzi   alipotembelea Kiwanda cha Korosho cha BUCO   Manispaa ya Lindi, ambako alishuhudia korosho zikipimwa ubora kwenye ghala kuu  kiwandani hapo.

Aliagiza semina ifanyike mwakani   maofisa ushirika baada ya kupata mafunzo wawasaidie wakulima kwenye msimu ujao watambue korosho walizopeleka kuziuza zina ubora gani.

Waziri Mkuu alisema katika semina hiyo wakutane maofisa kilimo na maofisa ushirika  wapate taaluma hiyo itakayowawezesha kupima korosho na kuitenga katika madaraja na kuwaondolea shida wakati wa mauzo.

Mrajisi Msaidizi wa Ushirika Mkoa wa Lindi, Robert Nsunza, alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba wataandaa semina hiyo kwa wahusika na kuanzia hapo wakulima watakuwa wakitambua ubora wa korosho zao kuanzia    vijijini.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Nangomba Holdings, Ramadhan Katau, ambaye ndiye mtunzaji wa ghala la korosho katika kiwanda cha BUKO, alisema ghala hilo lina uwezo wa kupokea na kutunza tani 10,000 za korosho.

Alisema hadi sasa tani zilizopo ghalani hapo ni 6,370 na    ukusanyaji wa korosho unaendelea kwa kuwa sasa ndiyo katikati ya msimu .

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,400FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles