24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa aonya viongozi wavivu na wala rushwa

Anna Potinus

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka viongozi kufanya kazi kwa juhudi na kuacha na tabia za uvivu na vitendo vya rushwa ambapo ameasa wananchi kutoa ushirikiano iwapoa watakutana na viongozi wa aina hiyo ili waweze kushugulikiwa.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Julai 20, alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kuzindua safari mpya ya treni ya mizigo ya Tanga – Kilimanjaro yenye mabehewa 20 yaliyokuwa na mzigo wa tani 800 za saruji kutoka kampuni ya Saruji ya Tanga.

“Serikali itaendelea kuwatumikia na mimi kama kiranja ninaagiza watumishi wenzangu tuchape kazi, mvivu, mwizi, mla rushwa muomba rushwa hana nafasi na ninyi wananchi msisite kutuambia ili tushughulike nao,” amesema.

Amesema kukamilika kwa kipande cha reli ya Tanga – Moshi na kuanza kutoa huduma ni mwendelezo wa utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya awamu ya tano kuhakikisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji inafaidika na fursa ya kijiografia iliyopo nchini kwa kutoa huduma za usafiri na uchukuzi wa reli kwa uhakika, usalama na kwa gharama nafuu.

“Wataalamu wa masuala ya usafirishaji duniani wanaeleza kuwa matumizi ya reli kwa ajili ya usafirishaji wa shehena, hupunguza gharama za bidhaa kwa asilimia kati ya 30 na 40, vilevile, matumizi ya reli huwa ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kutokana na ukweli kwamba, kupitia usafiri wa reli unaweza kusafirisha mizigo mingi kwa haraka na kwa wakati mmoja kwenda kwa mlaji,” amesema.

“Ninaagiza viongozi na watendaji wa mikoa na maeneo ambayo yanapitiwa na reli hii, kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania, waanze mara moja kampeni ya kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama lakini pia kuwakumbusha wananchi kuwa walinzi wa miundombinu hii muhimu ya reli,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles