31.3 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGWA MAJI MAREFU

Na NORA DAMIAN,DAR ES SALAAM


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani, maarufu kama Profesa Maji Marefu.

Akizungumza wakati wa ibada ya kuaga mwili huo iliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam jana, Majaliwa alitoa pole kwa wanafamilia na kuwaomba waendelee kumwombea marehemu apumzike mahala pema peponi.

Aliwaomba wanafamilia wawe watulivu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Naye Sheikh Ally Mkoyogole aliyeongoza dua ya kumuaga mbunge huyo kwa niaba ya Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubeiry bin Ally, alisema kila mtu anapaswa kujitafakari na kujiweka tayari.

“Ni lazima kuna siku tutakuwa hatupo katika ulimwengu huu, tuzingatie yanayopita ulimwenguni kwa fikra nzuri na tujihesabu wenyewe kabla hatujahesabiwa,” alisema Sheikh Mkoyogole.

Kaka wa marehemu, Hilary Ngonyani, alisema familia imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mtu muhimu.

“Kuondokewa na mtu wa aina hii katika familia wote tunajua, tumepata pigo kwa sababu alikuwa kiungo kikubwa. Tutajipanga ili aliyoyaacha katika familia yaweze kuendelezwa,” alisema Ngonyani.

Kwa habari kamili jipatie nakala yako ya  gazeti la MTANZANIA hapo juu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,507FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles