Majaliwa aitaka Ruvuma kutangaza fursa za uwekezaji

0
620
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kitabu cha muongozo wa uwekezaji katika Mkoa wa Ruvuma, kwenye maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma. Julai 25.2019. Tokea kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje John Ndumbalo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme

Anna Potinus

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameutaka uongozi wa mkoa wa Ruvuma uendelee kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo na kuondoa vikwazo vyote ili kuvutia wawekezaji zaidi.

Ametoa wito huo leo Alhamisi Julai 25, wakati akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji mkoani Ruvuma linaloendelea kwenye uwanja wa Majimaji, Manispaa ya Songea ambapo pia amezindua Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo.

“Nitoe rai kwa Mkoa uendelee kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo sambamba na kuondoa vikwazo vyovyote vya uwekezaji na biashara ili kuvutia zaidi wawekezaji wa ndani na nje kwani Mkoa wa Ruvuma kama ilivyo mikoa mingine, unazo fursa ambazo zikiendelezwa zitaleta tija na kusaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa letu.,” amesema.

Ametoa wito huo leo mchana (Alhamisi, Julai 25, 2019) wakati akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji mkoani Ruvuma linaloendelea kwenye uwanja wa Majimaji, Manispaa ya Songea. Pia amezindua Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo.

“Kongamano hili ambalo kaulimbiu yake ni Ruvuma itavuma kwa uchumi wa viwanda, wekeza sasa,” imelenga kutangaza fursa za uwekezaji na biashara zilizopo mkoani humu, na  inajipambanua vyema na kuendana na azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo 2025.”

Amesema mchango wa sekta ya viwanda kiuchumi na kijamii nchini ni pamoja na kuongeza pato la Taifa na kupandisha hali ya maisha ya wananchi pia kusaidia nchi isiyumbe kiuchumi ikizingatiwa kuwa viwanda vingi havitegemei hali ya hewa kama kilimo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here