25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa aitaka Hospitali ya Aga Khan kufanya mapitio ya gharama

FERDNANDA MBAMILA – Dar es Salaam

SERIKALI imeutaka Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) ufanye mapitio ya gharama za afya katika Hospitali ya Aga Khan ili wananchi wa kawaida wamudu kupata tiba wanazozitoa.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali hiyo.

Alisema upanuzi wa hospitali hiyo ni miongoni mwa jitihada za kuwafikishia Watanzania huduma za afya katika maeneo yao na kwa ngazi zote na kwa gharama nafuu.

Aliwataka watoa huduma wote nchini waangalie upya gharama zinazotozwa katika huduma mbalimbali hususani za matibabu.

 “Mtakubaliana nami kuwa gharama zikiwa kubwa hazitawanufaisha wananchi hususani wa kipato cha chini na wananchi hawataona unafuu wa kutibiwa nchini na nje ya nchi, hivyo fanyeni mapitio ya gharama hizo,” alisema.

Pia alisema Serikali inatambua gharama kubwa za uwekezaji na uendeshaji wa shughuli za afya nchini.

 “Lengo la Serikali kutoa misamaha ya kodi kwa baadhi ya taasisi zisizo za kiserikali kama Aga Khan ni kuwezesha huduma zinazotolewa kuwa nafuu,” alisema.

Pia alisema Serikali imeanzisha na kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na mwitikio ni mkubwa.

Alisema lengo ni kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya matibabu tena kwa uhakika.

“Nitoe wito kwa taasisi zote zisizo za Serikali kuunga mkono jitihada hizi na kuhakikisha wananchi wote wananufaika na huduma zenu kupitia mfumo huu bila kubaguliwa,” alisema.

Pia aliutaka uongozi wa Hospitali ya Aga Khan na NHIF ukamilishe majadiliano yao.

“Dk. Konga (Bernard Konga), Mkurugenzi Mkuu wa NHIF upo hapa kamilisheni mjadala,” alisema.

Pia alisema nia ya Serikali ni kuona wananchi wanakwenda hapo katika jengo hilo zuri na wanapata huduma kupitia bima ya afya.

“Ni matumaini yangu kwamba jambo hili litafanyiwa kazi kwa kuzingatia masilahi mapana ya pande zote mbili,” alisema.

Pia alisema Serikali itaendelea kuhakikisha uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji, kuimarisha amani na utulivu na alitoa rai kwa sekta binafsi ziendelee kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo nchini kwa kuzingatia sheria za nchi, utamaduni na mila za Watanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles