30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AINYOOSHEA KIDOLE TRA

Gabriel Mushi, Dodoma


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kuacha kutumia lugha chafu na nguvu katika ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara.

Pia amemwagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kukutana na uongozi wa mamlaka hiyo ili kuieleza umuhimu wa kuzingatia maadili na weledi katika ukusanyaji wa kodi.

Majaliwa ametoa maagizo hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu mbinu zinazotumiwa na TRA kukusanya kodi kwa kuwatoza kodi kubwa isivyo halali wafanyabiasha na wengine kupoteza maisha kwa mshtuko.

Mwakajoka alisema licha ya serikali kutekeleza sera ya viwanda, TRA inatumia mbinu za ovyo kukusanya kodi hali inayowalazimisha baadhi ya wafanyabiashara kuhamishia biashara zao nje ya nchi.

Akijibu swali hilo, Majaliwa alisema aliwahi kutoa maelekezo kwa TRA kutotumia nguvu na kubambikia kodi kubwa na kwamba iwapo wafanyabiashara watakuwa wana malalamiko, inabidi wayafikishe kwenye chombo cha kusikiliza malalamiko kilichopo ndani ya TRA.

“Lakini pia kama inapoonekana ndani ya TRA husikilizwi wizara ya fedha ipo na ndio yenye mamlaka na TRA yenyewe, wafanyabiashara pia wana uhuru mkubwa wa kwenda kwa kiongozi  mkuu wa eneo mkuu wa mkoa kwenye hilo ngazi mkoa au mkuu wa wilaya ngazi ya wilaya ili kulalamikia jamnbo hili na hatimaye mkuu wa mkoa unachukua hatua kujua kwanini kumejitokeza katika jambo hili.

“TRA fanyeni kazi yenu kwa weledi, endeleeni kuwa na mazungumzo na wafanyabiashara na sasa tunaona kila mmoja anaona umuhimu wa kulipa kodi,” amesema Waziri Mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles