22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

MAJAJI WAPYA WAPIGWA MSASA

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Majaji wapya 14 wamepigwa msasa katika semina ya mafunzo elekezi huku wakitakiwa kujipa muda wa kusoma majalada ya kesi  hususan za madai ambayo wakati mwingine hayahitaji kukaa muda mrefu na yanahitaji uamuzi mdogo yaishe

Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam leo Mei 7, katika ufunguzi wa mafunzo hayo na Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma na kuongeza kuwa Mahakama ya Tanzania inafanya kazi kwa mujibu wa sheria ya nchi hivyo lazima wajue malengo yao na kuelewa majukumu yao mahali popote wanapokuwa.

Amesema mafunzo hayo ni hatua ya kwanza kuelewa kwamba kazi ya ujaji inahitaji mafunzo endelevu kwa kuwa kuna waliokuwa mawakili wa kujitegemea, wasajili na kwamba kazi ya ujaji ni ya kipekee na si kazi rahisi.

“Natoa onyo kwa majaji wapya kujua kwamba hukumu zinapopatikana katika mitandao kosa moja litajulikana duniani kote.

“Zamani kulikuwa na dhana majaji wanajua sheria, lakini kuna mambo mengi ambayo hawakuweza kuyafanya wakati wanafundishwa sheria kuna matumizi ya Tehama, Sheria ya Mitandao hivyo elimu endelevu kwa majaji ina umuhimu sana,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles