24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Maiti zalazwa sakafuni hospitalini Misungwi

misungwi-hospital-11

Na JUDITH NYANGE,

MAITI mbili kati ya 13 zilizopatikana kutokana na ajali ya Hiace na basi la Super Shem wilayani Kwimba   zimehifadhiwa chini katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kwa vile  hospitali hiyo  haina  chumba cha kuhifadhia maiti.

Miili hospitalini hapo huhifadhiwa  katika chumba kidogo cha muda chenye uwezo wa kuhifadhi miili minne tu  kwa kulaza  sakafuni.

MTANZANIA ilishuhudia  maiti tatu zikiwamo mbili za ajali ya iliyohusisha basi la Super Shem   lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza na Hiace   iliyokuwa ikitoka Kata ya Shirima wilayani Kwimba, ikiwa imelazwa  sakafuni ndani ya chumba kidogo kinachotumia kuhifadhia maiti  Ajali hiyo  ilitokea katika  Kijiji cha Mwamaya.

Muuguzi Mkuu  wa Hospitali ya Wilaya Misungwi, Florah Kuzenza, alisema wanalazimika kutumia chumba kidogo   kuhifadhi maiti kwa dharura  kwa sababu  hospitali hiyo haina chumba wala vifaa vya kuhifadhi maiti.

“Maiti zinapopatikana tunalazimika kuzichoma  sindano ili zisiharibike na kuzihifadhi sakafuni katika  chumba tunachokitumia kama mortuary  hata maiti tulizozipokea mapema leo (juzi) asubuhi tumezihifadhi katika chumba hicho.

“Zinapopatikana maiti zaidi ya nne au inapotokea ajali kubwa na kuua watu wengi na maiti zikaletwa hapa, tunalazimika  kuhamisha vitu vilivyopo katika chumba cha wodi ya wanaume pamoja na wagonjwa na kuitumia wodi hiyo kuhifadhi maiti  hizo kwa kuzipanga sakafuni,” alisema Kuzenza.

Kuzenza alisema maiti inapopatikana wanajitahidi kutafuta ndugu wa marehemu  waweze  kuchukua miili za ndugu zao na zinazopatikana za kuokotwa barabarani na kuletwa hospitali zikaa zaidi ya siku mbili bila kutambuliwa hulazimika  kuomba kibali polisi na kuzika katika eneo la hospitali.

Alisema   kwa  Septemba pekee wameshazika zaidi ya maiti tatu katika eneo la hospitali baada ya kushindwa kutambuliwa na kukosa ndugu.

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda,    alisema  ofisi yake inalifahamu suala hilo na tayari wamepatikana wafadhili  na hivi sasa unatafutwa      ushauri na kuangalia vyumba vya kuhifadhia maiti vilivyopo katika  hospitali nyinginea ili    kuanza ujenzi Januari, 2017.

“Tunatafuta ushauri kutoka Hospitali ya Temeke, Amana na Muhimbili ili jengo tutakalojenga liwe la kisasa na liendane na wakati tuliopo,” alisema Sweda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles