24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

MAHALI WATAKAPOKUTANA TRUMP, KIM NCHINI SINGAPORE PAJULIKANA

WASHINGTON, MAREKANI


MKUTANO unaosubiriwa kwa hamu kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un utafanyika kwenye hoteli iliyopo Kisiwa cha Sentosa, Singapore, Ikulu ya Marekani imethibitisha.

Mkutano huo wa Juni 12, utakuwa wa kwanza kati ya Kiongozi wa Korea Kaskazini na Rais aliyepo madarakani Marekani.

Usiku wa kuamkia jana, Rais Trump alisema maandalizi ya mkutano yanaendelea vizuri.

“Uhusiano mwingi unaundwa, majadiliano makubwa yanaendelea kabla ya safari,” aliwaambia wanahabari usiku huo.

Lakini inavyoonekana ni kuwa watakaa katika hoteli tofauti za kisiwa hicho kikuu kati ya visiwa 63 vya Singapore, kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Straits Times.

Kwa ghafla, Kim Jong-un amekuwa kiongozi mpya mwenye umaarufu katika siasa za kimataifa mwaka 2018 baada ya kuwa kando kwa miaka mingi.

Hadi sasa ameshakutana au anatarajia kukutana na viongozi kutoka China, Urusi, Syria, Korea Kusini na Marekani.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin amemualika kukutana naye mjini  Vladivostock Septemba mwaka huu huku Rais wa Syria, Bashar al Assad akisema angependa kuitembelea Pyongyang.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,853FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles