29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yawaachia huru Wakurugenzi MSD, Logistiki

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na aliyekuwa Mkurugenzi wa Logistiki, Byekwaso Tabura wameachiwa huru baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutoa hati ya kuonesha hana nia ya kuendelea mashtaka hayo.

Uamuzi huo umetolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kassian Matembele baada ya upande wa mashtaka uliokuwa ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kuwasilisha hati ya kuonesha hawana ni ya kuendelea na mashtaka hayo iliyosainiwa Mei 10, 2021 na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Biswalo Mganga.

Hati hiyo ilisainiwa chini ya kifungu cha 91(1) cha sheria ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2019.

Katika kesi hiyo, washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo utakatishaji fedha haramu zaidi ya Sh bilioni 1.6.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ilidaiwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 30, 2019 katika maeneo mbalimbali ya jiji na mkoa wa Dar wa Salaam wakiwa watumishi wa umma kwa pamoja walitengeneza genge la uhalifu kwa ajili ya kujipatia faida.

Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa kati ya Julai 1, 2016 na June 20, 2019 washtakiwa wote kwa pamoja waliisababishia MSD hasara ya Sh 3,816,727,112.75.

Iliendelea kudaiwa kuwa Bwanakunu akiwa ni mtumishi wa umma alifanya matumizi mabaya ya madaraka kwa kongeza mishahara na posho za wafanyakazi bila ruhusa ya Katibu Mkuu Utumishi na kuisababishia MSD hasara ya Sh Sh 85,199,879.65 kosa alilodaiwa kulitenda Julai 1, 2916 na June 30, 2019 katika maeneo ya Keko wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam.

Pia ilidaiwa kati ya Julai 1, 2016 na June 30, 2019 katika maeneo ya tofauti ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania washtakiwa hao kwa pamoja waliruhusu uhifadhi mbaya wa vifaa tiba uliosababisha vifaa hivyo kuharibika na kuisababishia MSD hasara ya Sh 85,199,879.65

Katika shtaka la mwisho ilidaiwa kati ya Julai 1, 2016 na June 30, 2019 katika maeneo ya Keko Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar wa Salaam wote kwa pamoja walijipatia fedha Sh 1,603,991,095.37 wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu ambao ni kuongoza genge la uhalifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles