MAHAKAMA YATUPA MAPINGAMIZI KESI YA VISIMBUZI

0
1248

Na RAYMOND MINJA,IRINGAHatimaye Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, imekubali kusikiliza maombi ya kupinga amri ya kaondolewa Chaneli za ndani kwenye visimbuzi vya AZAM, DStv, ZUKU na  Star Times.

Maombi hayo yaliletwa mahakamani hapo na walalamikaji watano kwa niaba ya watumiaji wa visimbuzi ambao ni Silvanus Kigomba, Jesca Msambatavangu, Oliver Motto Sebastian Emmanuel, Atilio na Hamdun Abdallah, akisoma uamuzi huo jana Jaji Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,  Penterine Kente alisema mahakama haioni sababu ya kukubaliana na mapingamizi yaliyowekwa na Wakili wa serikali Mwinyiheri Aristaric.

Wakili huyo wa serikali aliiomba Mahakama hiyo kutupilia mbali maombi hayo yaliyoletwa na watu watano kwa niaba ya watumiaji wa visimbuzi hivyo.

Jaji Kente alisema kuwa hoja zilizoletwa na Wakili wa serikali ikiwemo kuomba Mahakama kutupa maombi hayo kwa kuwa muda wa siku 14 unaoitaka Mahakama kuanza kuyasikiliza umeshapita hakubaliani nayo.

Alisema hoja hiyo imejaribu kushawishi Mahakama kuwabebesha mzigo waleta maombi ambao wao waliyaleta ndani ya muda kisheria.

Maombi mengine ya Wakili wa serikali yalikuwa ni mahakama isisikilize maombi hayo kwakuwa waleta maombi wameshindwa kuwafikishia samansi baadhi ya washitakiwa na kusababisha kutokuwepo mahakamani.

Katika ombi hilo Jaji Kente alisema kuwa anakubaliana  na hoja za wakili wa waleta maombi, Edmund Mkwata aliyeomba hoja hiyo kutupiliwa mbali kwa kuwa mahakama hiyo inayo  ruhusa kisheria kusikiliza maombi hayo katika hatua za awali bila  upande mwingine kuwepo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here