27.4 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA YATAKA UPELELEZI KESI YA PEDESHEE NDAMA UKAMILIKE

Gavel-300dpi-Small

Na Kulwa Mzee -Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imeutaka upande wa Jamhuri kukamilisha haraka upelelezi katika kesi ya  kughushi, kutakatisha fedha na  kujipatia Dola za Marekani 540,390 kwa udanganyifu inayomkabili mfanyabiashara Ndama Shabani Hussein, maarufu kama Pedeshee Ndama Mtoto wa Ng’ombe (44).

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa, alisema hayo jana baada ya Wakili wa Serikali, Leonard Challo kudai mahakamani wakati kesi ilikuwa inatajwa, kuwa upelelezi haujakamilika.

Mwita aliomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.

Hakimu Nongwa, aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 24, mwaka huu na kuamuru upande wa mashtaka kuhakikisha upelelezi unakamilika haraka.

Awali ilidaiwa Februari 20, 2014 Dar es Salaam kuwa mshtakiwa alighushi kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonesha kuwa Kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment iliruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu kilogramu 207 yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000 kwenda Australia kwa Kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.

Mshtakiwa huyo, anadaiwa kuwa Machi 6, 2014, Dar es Salaam, alighushi kwa kutengeneza hati ya kibali (Certificate of Clearance) ya Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam akijaribu kuonesha kilo 207 za dhahabu kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), zinatarajiwa kusafirishwa na Kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment kwenda Australia kwa Kampuni ya Trade TJL DTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati akijua si kweli.

Inadaiwa Februari 20, 2014 mshtakiwa huyo anadaiwa kughushi fomu ya forodha yenye namba za usajili R.28092 akionesha Kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment imelipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) dola za Marekani 331,200 kama kodi ya uingizaji wa bidhaa ambazo zina uzito wa  kilogramu 207 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000 kutoka Kongo kitu ambacho si kweli.

Iliendelea kudaiwa kuwa Februari 20, 2014, mshtakiwa huyo alighushi nyaraka ya bima kutoka Phoenix of Tanzania Assurance  Company Ltd akionesha Kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited imeyawekea bima maboksi manne yaliyokuwa na dhahabu hizo zenye uzito wa kilogramu 207 wakati akijua ni uongo.

Kati ya Februari 26 na Machi 3, 2014 jijini Dar es Salaam kwa njia ya udanganyifu anadaiwa alijipatia kutoka kwa kampuni ya nchini Australia ya Trade TJL DTYL Limited dola za Marekani 540,390 baada ya kudanganya atawapa na kusafirisha dhahabu hizo zenye uzito wa kilogramu 207 na thamani ya dola 8,280,000 wakati akijua kuwa ni uongo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles