29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Mahakama yataka upelelezi kesi ya Lema ukamilishwe

godbless-lema-arushaNa JANETH MUSHI

-ARUSHA

HAKIMU Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Agustino
Rwizile, ameutaka upande wa Jamhuri katika kesi zinazomkabili Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema (Chadema), kukamilisha upelelezi wa kesi kabla ya kuzifikisha mahakamani.

Agizo hilo alilitoa mjini hapa  alipoahirisha kesi zinazomkabili Mbunge huyo anayetuhumiwa kusambaza ujumbe unaomkashifu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kuhamasisha wananchi kufanya maandamano Septemba Mosi, mwaka huu.

“Kuna maelekezo yametolewa baadhi ya kesi watu wa mashitaka mnatakiwa kuzileta mahakamani kabla hamjakamilisha upelelezi. Lakini pia kuna kesi kama hizi zilizopo mbele yetu mnatakiwa kuzileta mkiwa tayari mmekamilisha upelelezi,”alisema Rwizile bila kufafanua.

Agizo hilo la hakimu limetolewa  baada ya upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Jamhuri, Blandina Msawa kudai  kuwa upelelezi wa shauri hilo ulikuwa haujakamilika na hivyo kuomba tarehe nyingine.

Hakimu Rwizile aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 12 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Vilevile,  aliuagiza upande huo wa mashitaka kukamilisha upelelezi ili mtuhumiwa asomewe hoja za awali za mashitaka yanayomkabili.

Katika kesi hiyo,  e Lema anawakilishwa na Wakili, John Mallya na jana mtuhumiwa huyo hakuweza kufika mahakamani kutokana na wadhamini wake kusema kuwa yuko katika kikao cha Bunge Dodoma.

Pamoja na kutolewa kwa udhuru huo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Rwizile aliuagiza upande wa utetezi kuhakikisha mtuhumiwa huyo anafika
mahakamani tarehe iliyopangwa  asomewa hoja za awali za mashitaka yanayomkabili.

Inadaiwa kuwa kati ya  Agosti 20, mwaka huu ndani ya Arusha,   mtuhumiwa huyo alituma ujumbe kutoka namba 0764150747 kwenda namba 0766-757575 uliokuwa ukidai, “Karibu, tutakudhibiti kama Uarabuni wanavyodhibiti mashoga.”

Katika kesi ya pili Mbunge huyo anadaiwa kati ya Agosti Mosi hadi 26, Mwaka huu alirusha maneno ya sauti kwa njia ya mtandao wa WhatsApp yenye ujumbe uliokusudia kuishawishi jamii   iandamane Septemba Mosi Mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles