25.7 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Mahakama yamtia hatiani Malkia wa meno ya tembo

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi hii imemtia hatiani malkia wa meno ya Tembo, Yang Feng Glan na wenzake wawili.

Hukumu hiyo imesomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye amesema Jamhuri wamethibitisha, ushahidi inajitosheleza kwamba washtakiwa walitenda makosa hayo.

Hakimu Shaidi aliwatia hatiani na kusema kwamba walifanya dharau kubwa kutumia maroli ya Serikali kubebea meno ya tembo kupeleka bandarini.
Alisema Mahakama ilifika katika shamba Muheza Tanga ambapo mshtakiwa wa pili alikuwa analima pilipili na humohumo ndiko walikokuwa wanafukia meno ya tembo, wanafukua na kuyasafirisha Dar es Salaam.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni raia wa China, Yang Feng Glan(66), Salvius Matembo Philemon Manase Katika kesi hiyo upande wa Jamhuri ulikuwa na mashahidi 11 wa upande wa utetezi, washtakiwa walijitetea wenyewe.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na biashara haramu ya Meno ya Tembo yenye thamani ya Sh bilioni 13 kinyume cha sheria.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao, wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22, 2014.

Katika shtaka la kwanza, washtakiwa katika kipindi hicho walifanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1889, vikiwa na thamani ya Sh bilioni 5.4 bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,897FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles