22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA YAMTAKA AG ATOE MAJIBU KESI YA UHURU WA KUJIELEZA, DEMOKRASIA

PATRICIA KIMELEMETA NA MANENO SELANYIKA -DAR ES SALAAM


MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imetoa amri ya kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) Kuwasilisha majibu ya waleta maombi katika mashauri mawili ya kikatiba yaliyowasilishwa mahakamani hapo ifikapo Machi 21 mwaka huu.

Mashauri hayo pamoja na mambo mengine, yanapinga namna Demokrasia ya vyama vingi, uhuru wa kujieleza na kukusanyika unavyokiukwa hapa nchini.

Mashauri hayo mawili ambalo moja ni namba 4/2018 na lingine namba 8/2018, yanasikilizwa mbele ya  jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Kiongozi,Ferdinand Wambari, ambayo pamoja na mambo mengine, yanahoji namna ya utendaji wa vyombo vilivyoundwa Kwa mamlaka ya kikatiba vinavyokiuka Katiba.

Hata hivyo mahakama hiyo jana iliahirisha mashauri hayo hadi Aprili 5, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena baada ya majaji wengine kutokuwepo mahakamani hapo kutokana na majukumu mengine ya kikazi.

Akizungumza na Wandishi wa habari nje ya mahakama hiyo Wakili Jebra Kambole, ambaye anawatetea waleta maombi wa shauri namba 4/2018 ambao ni  Francis Galatwa, Baraka Mwango na Allan Bujo, alidai kuwa, wateja wake wanapinga kifungu namba 11 cha sheria ya vyama vya siasa ambacho kinatumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwateua Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

“Kimsingi kifungu hiki kina upungufu wa sheria ndio maana suala hili tumelileta mahakamani kwa ajili ya kupata ufafanuzi,” alidai Kambole.

Alidai ukisoma sheria hizo unaona wazi kuwa zina upungufu kwenye baadhi ya vipengele vyake ambapo wananchi wakifanya maandamano mwisho wa siku huleta madhara sio tu kwa waandamanaji bali kwa wengine ambao wameitwa na viongozi kwa ajili ya kuhudhuria.

Shauri namba 8/2018, ambalo limewasilishwa na mleta maombi Bob Chacha Wangwe  ambaye anatetewa na wakili Fatuma Karume,analalamikia kifungu namba 43,44,45 na 46 ambavyo vinatumiwa na jeshi la Polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano.

Katika shauri hilo pia,Wangwe anamlalamikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG). Majaji wengine wanaosikiliza shauri hilo na Jaji Temba na Jaji Sameji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles