31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Mahakama yamshauri DPP kuiondoa kesi ya uamsho, yaondoa zuio waandishi kuripoti

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), ameshauriwa kukamilisha upelelezi ndani ya muda mfupi ama kuiondoa mahakamani kesi ya ugaidi inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake 22 .

Mahakama imefikia uamuzi huo leo asubuhi wakati kesi hiyo ilipokuja mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Maira Kasonde kwa ajili ya kutajwa na uamuzi wa maombi yaliyowasilishwa na washtakiwa kupitia mawakili wao.

Washtakiwa kupitia mawakili wao, Abubakar Salim, Juma Nassoro na wengine waliwasilisha maombi mawili mahakamani ambapo ombi la kwanza walitaka mahakama imshauri DPP kukamilisha upelelezi ndani ya mwezi mmoja na ombi la pili mahakama iondoe amri ya kuwazuia waandishi wa habari kuripoti kesi hiyo.

Akitoa uamuzi Hakimu Maira alisema mahakama inampa njia mbili DPP, moja kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo ndani ya muda mfupi na njia ya pili kama anaona kuna sababu za upelelezi kuchelewa kukamilika aliondoe shauri hilo mahakamani na atakapokuwa tayari atawashtaki tena.

“Katika maombi ya kuondoa amri ya  kuripoti  kesi hiyo, mahakama inaondoa amri hiyo, Mahakama Kuu ndiyo inaweza kutoa amri kwa sababu sheria inazuia kuandika jina na kutoa picha ya shahidi wakati wa usikilizaji wa kesi ambapo hatua hiyo kesi inakuwa huko kwa usikilizwaji,” amesema.

Washtakiwa hao wako ndani tangu mwaka 2014 waliposhtakiwa kwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi ambapo mahakama hiyo iliamuru waandishi wa habari kutoripoti shauri hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles